Na David John, TimesMajira Online, Geita.
BAADHI ya wananchi wa mkoa wa Geita wamesema, kupitia Maonyesho ya tatu ya uwekezaji wa teknolojia ya Madini mkoani humo, wamenufaika na upatikanaji wa vitambulisho vya Bima ya Afya kwa urahisi ukilinganisha na huko nyuma.
Wakizungumzia hilo leo, baada ya kukabidhiwa vitambulisho hivyo na mkuu wa wilaya ya Geita Fadhili Juma. kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Mhandis Robart Gabriel chini ya usimamizi wa Meneja wa Bima ya Afya mkoa wa Geita Elius Othiambo amesema, hivi Sasa wanauhakika wa kupata huduma mahala popote ndani ya nchi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mara baada ya kupokea vitambulisho hivyo vya Bima ya afya kwa watoto kutoka NHIF kwenye viwanja vya maonyesho ya sekta ya madini yanayoendelea mkoani humo, Rehema Elikana mkazi wa katoro. amesema, wamefurahi kuona watoto wamepata vitambulisho ambavyo vitawezesha kupata matibabu kwa urahisi.
Amesema, awali walikuwa wanakutana na changamoto za matibabu hasa mtoto akiumwa na kupelekwa Hospitali walikuwa wanakutana na gharama kubwa za matibabu hali iliyo kuwa inasababisha watoto na hata wakubwa kutokupata huduma kwa wakati.
Naye Sufian Hassan mkazi wa mkoani Geita amesema, wanajisikia faraja kupata vitambulisho hivyo kwa ajili ya matibabu kwa watoto wao Jambo ambalo litarahisha upatikanaji wa huduma .
“Tunaishukuru Sana Serikali kupitia NHIF) mfumo wa Bima ya afya mkoani Geita kwa kutuwezesha kupata vitambulisho hivi kwa ajili wa watoto wetu .tunashukuru Sana.”amesema Hassan
Kwaupande wake Meneja mfuko sa Bima ya Afya Mkoa wa Geita Elius Othiambo amesema, kupitia Maonyesho hayo wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo upimaji wa kipimo cha uwiano wa uzito na utefu, kisukari, HIV, ugonjwa wa moyo pamoja na magonjwa mengine.
Pia amesema, walikuwa na uelemishaji wa Jamii kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko wa bima ya afya pamoja na kufanya uwandikishaji wa papo kwa papo na mwitikio wa kujiunga wanachama kwenye Banda lao umekuwa mkubwa na kufikia wanachama 150 waliojiandikisha kupitia kwenye Banda hilo.
“Leo kumekuwa na hafla ya kukabidhi kadi za Mfuko wa Bima ya Afya NHIF ambazo zinaitwa Toto afya kadi kwa watoto wenye umri chini ya miaka18 na kadi hizi zimekabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Geita mjini Fadhili Juma kwaniba ya mkuu wa mkoa mhandis Robart Gabriel.”amesema Othiambo.
Othiambo ameongeza, “NHIF ni kwakila mtu yaani kwa makundi yote, iwe ni boda boda, wakulima, wafanyakazi, wavuvi, wafanyabiashara, wachimbaji madini, nawatumishi waserikali ,”amesisitiz Othiombo.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Fadhili Juma kwaniaba ya Mkuu wa mkoa Mhandis Robart Gabriel amesema, anaishukuru Serikali ya awamu ya tano Kwa kuja na sera ya kuja na mpango wa bima ya Afya (NHIF) .
“Ndugu zangu mpango huu ni madhubuti, imara ambao umeandaliwa Kwa ajili ya kulinda Afya ya mwananchi, mpango huu unalengo zuri kwa raia na unamwezesha mwananchi kutibiwa kwenye hospitali yeyote ile hapa nchini .”amesema Mkuu wa Wilaya hiyo.
Amefafanua kuwa, hospitali hizo iwe za mtu binafsi, rufaa, au serikali kwa gharama nafuu kabisa ya shilingi 50, 400 utakuwa na uhakika wa Afya yako kutibiwa kwa muda wa mwaka mzima ndani ya nchini.
Maonyesho hayo yameweza kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo wakuu wa Mikoa wa Mara Adam Malima, Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongela, Mkuu wa Mkoa Shinyanga Zainab Telack, pamoja na makatibu wakuu wa wizara mbalimbali na kilele cha maonyesho hayo kitafungwa na Waziri Mkuu Majaliwa kassim Majaliwa Septemba 27 mwaka huu.
%%%%%%%%%%%%%%
More Stories
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali
Walimu S/ Sekondari Ilala wafundwa juu ya maadili ya wanafunzi