Na Mwandishi Wetu, TimesmajiraOline, Kagera
JANA, Februari 27, 2024 ilikuwa siku ya furaha, nderemo na vifijo kwenye Shule ya Sekondari ya Bukoba Hope, ambapo Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu/Idara ya Huduma za Jamii na Mratibu wa kitengo cha elimu, alikubali mwaliko wa ziara ya pongezi kwa shule hiyo kufanya vizuri mitihani ya taifa kidato cha pili na cha nne mwaka 2023.
Tukio hilo la furaha liliambatana na matukio ya Show, ngoma na utoaji
zawadi kwa wanafunzi washindi ambao wameingia kidato cha tatu kwaka huu.
Aidha, zawadi zilitolewa kwa walimu na wafanyakazi ambao sio walimu.
Tukio hilo pia lilikolezwa na tukio la shule kufanya uzinduzi wa Program ya E-learning, ambapo vilizinduliwa vishikwambi vyenye program ya masomo ya kidato cha kwanza.
Kupitia vishikwambi hivyo vitawawezesha wanafunzi kusoma topic hata bila mwalimu kwa kuona clips na vitabu vilivyo ndani ya vishikwambi hivyo.
Program hii imehamasishwa na Shirika la Education Opportunity lililoko Arusha.
Hakika, Tunawapongeza Bukoba Hope kwa ushindi mnono na tunaitia moyo
ili izidi kufanya vizuri zaidi.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua