Na Jackline Martin, TimesMajira Online
TUME ya Ushindani (FCC) imeomba Serikali kupitia mamlaka zake kuweka utaratibu wa kiudhibiti utakaowataka watoa huduma kupitia mfumo ya teknolojia kuweka bayana changamoto zinazoweza kujitokeza kwa walaji wanapotumia teknolojia na namna wanavyoweza kuzitatua changamoto hizo.
Pia imezitaka Mamlaka za usimamizi wa soko ikiwemo FCC na Mamlaka nyingine zinazosimamia mifumo ya teknolojia kukaa pamoja na kujadili ili kuja na mapendekezo ya namna bora zaidi ya kusimamia eneo hilo.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani (FCC), Dkt. Aggrey Mlimuka, wakati wa kongamano la matumizi ya akili mlemba yanayozingatia haki na uwajibikaji kwa mlaji lililoenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘Matumizi ya Akili mnemba yanayozingatia Haki na Uwajibikaji kwa Mlaji.
“Sote tuna shauku ya kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa ubora zaidi kwa walaji kwa kutumia teknolojia kama nyenzo muhimu kwa ustawi wa maslahi ya walaji na uchumi kwa ujumla, lakini azma hiyo itakuwa na maana pale ambapo mifumo hii ya kiteknolojia itazingatia uwajibikaji, tija, haki na usawa kwa kuwekewa mifumo thabiti ya usimamizi na udhibiti “
Pia Mlimuka amesema kuwa matumizi ya akili mnemba katika huduma za malaji ni vyema yabainishwe faida na athari hasi ili kuwezesha watunga sera, sheria, mifumo ya usimamizi na uthibiti pamoja na watafiti kuthibitisha faida na hasara zilizopo na kuwezesha kubuniwa kwa taratibu zitakazohakikisha kuwa matumizi ya Akili Mnemba katika huduma za walaji yanazingatiwa misingi ya sheria, taratibu, na kanuni za kumlinda mlaji na maslahi mapana ya mlaji.
“Walaji wana hofu namna ya mifumo huduma inayotumia akili mnemba namna inavyoundwa,” amesema
Aidha, amesema katika utekelezaji wa jukumu la msingi la kumlinda mlaji katika uchumi wa soko nchini Tanzania, amesihi kuundwa kwa mifumo ya huduma inayotumia Akili Mnemba
“Walaji wanahofu kuhusu namn ambavyo mifumo huduma inayotumia Akili Mnemba inavyoundwa, tunapaswa kuhoji na kutafiti namna ambavyo mifumo hii inaundwa na kusimamiwa na endapo haya yanafanyika kwa namna inayolinda maslahi ya mlaji,”amesema.
“Utafutaji na utumiaji wa taarifa za walaji ufanyike kwa ridhaa ya watumiaji, bila ulaghai na taarifa hizo zisitumiwe vibaya,” Alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ushindani (FCC), William Erio, amesema kongamano hilo limekutanisha waatalumu wa mifumo kutoka sekta za benki, usafirishaji pamoja na sekta nyingine za huduma.
Amesema kuwa wadau hao watajadili kwa pamoja kuona namna gani wataweza kutekeleza haki za mlaji katika mazingira ya matumizi ya akili mlemba na kama kutakuwa na kikwazo cha kisheria hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kupitia taratibu za kiserikali na kuhakikiha matumizi ya akili mlemba yanatumika kisheria na walaji wanalidwa.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa