Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
TAASISI ya Fahari Tuamke Maendeleo iliyopo wilayani Ilala kata ya Gongolamboto inatarajia kuzindua kituo kinachojihusisha na Ujasiriamali,mazingira, jinsia na afya January 27 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa taasisi ya Fahari Day Care center Neema Mchau alisema uzinduzi huo unatarajia kufanyika kata ya Gongolamboto kitahusisha makundi ya vijana ,wanawake na wasichana walio nje ya mfumo wa shule.
“Taasisi yetu inazindua kituo cha mazingira jumamosi January 27 mwaka huu ambacho kitashugulika na makundi mbalimbali yakuwemo ya wanawake, vijana na wasichana dhumuni la mafunzo hayo kutoa elimu na kutengeza ajira ili makundi hayo kuyajengea uwezo waweze kupata fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi “alisema Neema.
Neema Mchau aliwataka vijana mbalimbali kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi kwa ajili ya kupata elimu hiyo ambayo itawakwamua kiuchumi kwa ajili ya ajira .
Alisema dhumuni la kuzindua mpango huo baada kuona makundi ya vijana wengi hawana shughuli maalum ambapo fursa ya mafunzo hayo ya Afya,ujasiriamali,mazingira yatawawezesha kujiajili wenyewe au kuajiliwa.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa