Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
KITUO cha Fahari Day Care kimeanzisha ahule ya Msingi, kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya Elimu nchini.
Shule hiyo ya msingi ni sehemu ya mafanikio ya Fahari Day Care ambapo kwasasa imetimiza miaka tisa toka kituo hicho cha kulea watoto kuanzishwa.
Akizungumza katika mahafali ya tisa ya Fahari Day Care Mkurugenzi wa kituo hicho Neema Mchau, alisema shule hiyo ya msingi inajulikana Fahari Elite Pre and Primary school, ipo kata ya Msongola Mtaa wa Kiboga wilayani Ilala.
“Kwa kutambua umuhimu wa elimu na kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan , tumewekeza sekta ya Elimu kwa kuanzisha shule ya Msingi ya kisasa ambapo wameanza na madarasa matatu ya awali na madarasa manne ya shule ya Msingi, vyoo matundu 16 jiko na ukumbi wa kulia chakula ,ofisi ya walimu na chumba cha maktaba vimekamilika taratibu za usajili zipo katika hatua za mwisho ambapo Mwenyezi Mungu akipenda January 2024 watoto wataanza rasmi darasa la kwanza “alisema Neema.
Mkurugenzi Neema Mchau alisema Fahari Day Care and Nurcery School ni mahafali ya tisa kituo kilianzishwa mwaka 2014 ni mmoja ya mradi ulipo chini ya Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo ikiwa na lengo la kusaidia jamii kwa kutoa elimu bora yenye malezi mema kwa watoto kwa kuzingatia utamaduni wa kitanzania ,pia kutumia mradi huo wa Fahari fursa ya kufikia jamii na kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Akizungumzia mafanikio kituo kimefanikiwa kusomesha watoto 15 wenye mahitaji Maalum kuanzia mwaka 2016 mpaka sasa bila malipo yoyote kuanzia elimu ya awali na sasa tumeshirikiana na Wazazi wapo shule za msingi za Serikali.
Akizungumzia Kitaaluma Fahari Day Care kimefanikiwa kutoa elimu bora kwa watoto na kuwafundisha wanafunzi kwa ufasaha na matokeo ya watoto yamekuwa mfano dhabiti huko mtaani sababu ya kuajili walimu bora wenye uzoefu wa kutosha kwenye ufundishaji .
Akizungumzia changamoto baadhi ya Wazazi kutofatilia maendeleo ya watoto wao Kitaaluma, na kinidhamu na baadhi ya Wazazi wamekuwa wazito kulipa ada kwa wakati hali inayopelekea shule kutofikia malengo yake.
Aidha migogoro ya familia Wazazi nyumbani inapelekea watoto kurudi nyuma Kitaaluma na kukosa haki zao za msingi
More Stories
Makalla: CCM tumewekewa mapingamizi,tunaamini haki itatendeka
Ilala kutoa mikopo ya shilingi bilioni 14
Rais Samia aipa TANROADS bil. 500/- ujenzi miundombinu Dar