November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Fahari Day Care waadhimisha siku ya mtoto wa Afrika

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

TAASISI ya Fahari Tuamke Maendeleo (Fahari Day Care)imeadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kata ya CHANIKA Wilayani Ilala kwa ajili ya kuwakumbuka mauaji ya watoto zaidi ya 2000 yaliofanywa na Utawala wa Makaburu katika kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini Juni 16/1976.

Katika Madhimisho hayo Fahari Day Care walishirikiana na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Ofisi Mkurugenzi pamoja na shule za Msingi za Kata ya CHANIKA ,shule ya Msingi Yongwe na Shule ya Msingi Virobo ambapo mgeni rasmi Mwenyekiti wa ccm kata ya Chanika William Mwila.

Risala ya watoto wa shule ya Msingi Yongwe iliyosomwa katika madhimisho hayo walisema Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo iliwaunganisha Wadau wa Ustawi wa watoto ,Wazazi na Walezi wa watoto katika kata ya CHANIKA ili kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika Dunia Juni 14 mwaka huu 2024

Watoto hao walisema madhimisho hayo yatakuwa endelevu kwa kushirikisha jamii ya eneo hilo na shule za msingi za jirani .

Akisoma risala hiyo alisema Juni 16 kila mwaka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika ikiwemo TANZANIA huadhimisha siku ya mtoto wa Afrika Dunia alisema chimbuko la siku hiyo ni mauaji ya watoto takriban 2000 uliofanywa na Utawala wa Makaburu katika kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini Juni 16 /1976 ambapo mauaji hayo yalitokea wakati wa maandamano ya wanafunzi kwa lengo la kupinga mfumo wa sekta ya Elimu wa kibaguzi uliokuwa ukitolewa na mfumo wa Elimu ya Kibaguzi uliokuwa ukitolewa na Utawala wa Afrika Kusini.

Akizungumza katika madhimisho hayo Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau, alisema siku ya mtoto wa Afrika huambatana na kauli mbiu inayolenga kuwasaidia watoto na ujumbe wa mwaka huu umebeba kauli mbiu isemayo “Elimu Jumuishi kwa watoto izingatie maarifa Maadili na stadi za kazi ambapo alisema kauli mbiu hiyo inaimiza utoaji wa elimu inayojumuisha watoto wote isoyobagua mtoto kutokana na hali yake.

NEEMA MCHAU alisema Elimu hiyo inalenga kumptatia mtoto maarifa (Elimu na Ufaulu)maadili mema ,uadilifu na hofu ya Mungu )Stadi za kazi (Kazi za mikono ili kujenga ujuzi kulingana na umri wa mtoto)

“FAHARI TUAMKE MAENDELEO tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza sekta ya Elimu msingi na Elimu Sekondari amejenga shule za kutosha katika nchi yetu na sisi Fahari tunaunga mkono juhudi zake Tumejenga shule za kisasa darasa la awali na shule ya Msingi “alisema Neema.

Aidha pia alipongeza uongozi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Ofisi Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii na idara ya Ustawi wa Jamii kwa ushirikiano wao mkubwa.

Alisema Fahari Day Care inaungana na Rais Samia katika sekta ya Elimu kuwekeza na kutoa elimu bora ili tuweze kulea jamii bora na kuwataka Watanzania kulea watoto katika misingi bora wasiingie katika mmomonyoko wa maadili

AFISA Maendeleo ya Jamii kata ya Chanika IDDA MDIMI aliwataka wazazi kutimiza wajibu wao katika kulea watoto watafute pesa na kulinda watoto katika maadili mema ili wawe watoto wa kizazi bora.