Na Joyce Kasiki,Timesmajira ,Dodoma
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imesema,inaendelea kuhamasisha wananchi kuwekeza kwenye eneo la matumizi ya ujenzi wa vituo vya kujaza gesi asilia kwenye magari (CNG).
Hayo yamesemwa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA Titus Kaguo wakati Naibu Waziri Mkuu alipotembelea kwenye banda hilo wenye maonesho ya Wiki ya Nishati Bungeni jijini Dodoma.
Amesema wadau wamekuwa na wasiwasi kuwekeza katika biashara hiyo kutokana na upya wake ndio maana kasi ya kuwekeza kwenye eneo hilo imekuwa ndogo.
“Ni kweli kasi ya kutoa vibali vya CNG ni ndogo lakini hii inatoana na mfumo ambapo kwanza ,biashara hii ni mpya watu wanajiuliza kwenye uwekezaji, ingawa sisi kama EWURA tumekuwa tukihamasisha sana na hadi sasa kuna kampuni kama 20 wameshonesha nia ya kuwekeza,lakini kikubwa bado wanajiuliza kama biashara inalipa.”amesema Kaguo
Amesema kutoana na hamasa ambayo wameendeea kuitoa wa wadau hali ya kurekebisha magari imeanza kufanyika wa kasi tofauti na huko nyuma.
“Mpaka mwaka jana magari yaliyokuwa yamerekebishwa yalikuwa kama 3000 tu,lakini mpaka sasa ni magari 4500yamesharekebishwa,kwa hiyo kasi ya kurekebisha magari imekuwa ni kubwa hata kampuni zinazorekebisha magari sasa hivi zimeongezeka zimefikia kumi ,kwahiyo tunachokifanya sisi ni kuhamasisha zaidi .”amesema Kaguo na uongeza kuwa
“EWURA tumekaa na Wakala wa Vipimo (TBS) kurekebisha ‘standards’ za vituo vya mafuta kwamba mtu yeyote mwenye kituo cha mafuta ya petrol anaweza kufanya CNG ,zile standards zimekuwa conveterd ili watu waombe.”
Kaimu Mkurugenzi wa Gesi asilia Mhandisi Poline Msuya amesema,kati ya waombaji 30 waliopewa vibali na Shirika la Petroli nchini (TPDC) kwa ajili ya kuleta maombi ya vibali vya gesi asilia, ni maombi sita tu ndiyo yapo EWURA kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
“Kwa hiyo kwa sasa maombi yaliyopo kwa ajili ya kufanyiwa kazi ni sita na wengine wamekwama kwenye kubadilisha matumizi kwani wanatakiwa wafanyiwe tathimini upya ya vituo vyao ili waweze kukidhi vigezo ,na tunawafuatilia kwa karibu.”amesema Kaimu Mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa
“Kuna watu mpaka sasa wameshanunua vifaa vya kufunga CNG mwaka mzima umeisha wapo navyo nyumbani ,hawawezi kufunga kwa sababu hawajatimiza takwa la cheti cha mazingira.”
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa