Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kanda ya kaskazini imewataka wafanyabiashara wa mafuta kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu za biashara hiyo na kuachana na tabia ya kuficha mafuta kwani kwa kufanya hivyo wana kiuka taratibu
mbali na hayo pia mamlaka hiyo imewataka wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanakuwa na mikataba ambayo itaweza kuwasaidia kupata mafuta kwa uraisi
hayo yameelezwa na Meneja wa Ewura Kanda ya kaskazini, Mhandisi Lorivii Lon’gidu alipokuwa akizungumza na wamiliki wa vituo vya mafuta Kanda ya kaskazini jijini Arusha mapema juzi.
aliongeza kuwa ni muhimu kwa wafanyabiashara wa mafuta kuhakikisha kuwa wanakuwa waaminifu ikiwa ni pamoja na kutoficha mafuta hali ambayk wakati mwingine husababisha madhara kwa watumiaji wa mafuta
“ni muimu sana kwa wafanyabiashara wa mafuta kuhakikisha kuwa sasa kila mmoja anafuta kanuni n sheria na pia tutambue kuwa mfanyabiashara mmojawapo anapokiuka sheria anasababisha shida kubwa na tusikubali hilo kabisa”aliongeza
mbali na hayo alisema mamlaka hiyo inawataka wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanauza mafuta bila kuwa na upendeleo wa aina yoyote
“huduma ya mafuta inatakiwa ifike kila maali kusiwepo na changamoto ya aina yoyote ile kwa kuwa mpaka sasa mafuta hasa kwa kanda ya kaskazini yapo tena ya kutosha”alisema
Alimalizia kwa kusema kuwa mamlaka hiyo sasa itaendelea kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara ikiwa ni kwa ajili ya kukumbushana umuhimu wa kufuata sheria na kanuni za uuzaji wa mafuta.
More Stories
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake