January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Eswatini kujifunza uendeshaji wa mifuko kutoka PSSSF

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

UJUMBE wa watu tisa kutoka Ufalme wa Eswatini, ukiongozwa na Mhe. Mabula Maseko, Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma, umetembelea Makao Makuu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishji wa Umma (PSSSF) jijini Dodoma Julai 19, 2024, kwa lengo la kujifunza masuala ya uendeshaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.


Taarifa ya PSSSF iliyotiwa saini na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama PSSSF, Bw. Yesaya Mwakifulefule imesema, Mhe. Maseko, amefuatana na waheshimiwa Wabunge na Watendaji wa sekta ya Hifadhi ya Jamii ambapo ujumbe huo ulipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru.


Taarifa imesema, PSSSF umekuwa ni Mfuko kivutio kwa taasisi za hifadhi ya jamii kutoka nchi mbalimbali kutokana na utendaji wake thabiti na unaoridhisha.


“Ufanisi na ubora wa huduma zinazotolewa PSSSF vimekuwa sababu kubwa ya kuwavutia wageni kutoka nje ya nchi kuja kujifunz,” taarifa hiyo iemsema.


Taarifa imezitaja nchi nyingine zilizowahi kuja kujifunza PSSSF ni pamoja na Uganda na Kenya.