January 19, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Emirates kuanzisha huduma ya abiria kuagiza mlo kabla ya safari

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Emirates imeanza hatua ya kwanza katika mpango wa ubunifu wa kuandaa chakula, ambapo wateja wataweza kuchagua chakula watakachotumia safarini kati ya siku 14 na masaa 24 kabla ya safari, hii ni kwa ajili ya kuhakikisha wasafiri wetu wanapata chaguo lao la chakula walichoomba kuandaliwa kwa wakati, na pia kusaidia kupunguza upotevu wa chakula.

Mpango huo utatekelezwa kuanzia tarehe 25 Julai na kuendelea katika Business Class, kwa safari zote za ndege kati ya Dubai na London Heathrow, London Gatwick na London Stansted, na kuongeza manufaa zaidi kwa uzoefu wa wateja wa Emirates, kuboresha usimamizi wa muda na kuongeza safu nyingine ya maarifa kuhusu matumizi ya chakula ndani ya ndege.

Kuagiza mapema mlo kutaongezwa kwa safu iliyopo ya data ya ufuatiliaji wa mteja iliyo wezeshwa na AI na ripoti za wafanyakazi , ambayo hurahisisha upangaji wa menyu na upakiaji bora wa chakula na huduma ya kisasa na hadhi ya chakula angani.

Siku 14 kabla ya safari, abiria wataweza kujivinjari kwa kuandaa menyu ya mtandaoni kupitia Emirates.com au katika program App ya Emirates na ili uchague mlo utakaokufaa uliozingatia tamaduni, radhaa za asili na viungo.Abiria pia anaweza kuagiza chakula maalum ikiwa atahitaji.Kwenye ndege, wahudumu wa ndege watatumia programu maalumu iliyoandaliwa katika kifaa ili kutazama uteuzi wa chakula na kumhudumia abiria chaguo lake.

Emirates ina mipango wa kupanua mpango huu wa kuagiza chakula kwa kuongeza safari nyingine na kuongeza madaraja katika siku za usoni na inafuatilia kwa karibu maoni ya wateja katika huduma hii kwa awamu ya kwanza.

Ubunifu wa huduma ya kuagiza chakula mapema ni nyongeza nyingine ya huduma ambayo itaongeza urahisi wa safari unaowezeshwa kidijitali ambao abiria wa Emirates hufurahia.

Pamoja na kuingia kwenye tovuti na kwenye programu, chaguo la pasi za kusafiria kidijitali na usimamizi wa ratiba, abiria wanaweza pia kufikia menyu dijitali mapema, kwa kujiunga na Emirates Skywards ili kufikia muunganisho wa bure mara moja kulingana na uanachama wa daraja na aina ya usafiri, na kutumia muda wa kutayarisha orodha ya filamu za kuonyesha zinazopendwa, vipindi vya televisheni na muziki, ambayo wanaweza kusawazisha kutoka kwenye programu yao hadi kwenye skrini ya televisheni yao pindi wakiwa safarini.

Abiria wa Emirates pia wamealikwa kukagua vipengele vyote vya safari zao za ndege katika uchunguzi wa haraka wa kidijitali unaoonekana kwenye skrini ya burudani ya ndege, kutoa maoni na maarifa ambayo yanahakikisha wateja wanasafiri vizuri zaidi wakitumia Emirates.