Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Taarifa za utafiti zilizotolewa na Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Utunzaji wa Rasilimali za Uvuvi (EMEDO) zinabainisha kuwa zaidi ya wavuvi 100,000 wanaofanya shughuli zao na kuishi pembezoni mwa Ziwa Victoria, kati yao 231 hupoteza maisha kwa mwaka kwa kuzama majini.
Hivyo ili kuhakikisha wavuvi wanakuwa salama
zaidi ya bilioni 2.7 zinatarajiwa kutolewa kutekeleza mradi wa kupunguza hatari za kuzama majini kwa jamii ya wavuvi walioko katika mikoa ya Mwanza, Kagera na Mara.
Ambapo mradi (mkakati)huo wa kupunguza ajali majini unatekelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na taasisi kutoka Uingereza inayohusika na masuala kwenye maji na uokoaji RNLI ambao wameingia mkataba wa miaka mitatu kusaidia jamii ya wavuvi.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa EMEDO Editrudith Lukanga wakati akizungumza na waandishi wa habari walipomtembelea ofisini kwake jijini Mwanza.
Ambapo ameeleza kuwa matukio ya ajali za majini yamesahaulika na hakuna jitihada za kimakusudi kuhakikisha ajali hizo zinapunguzwa tofauti na ajali za barabarani na zingine zinavyochukuliwa kwa uzito.
Lukanga ameeleza kuwa ajali za majini hazijawahi kupewa kipaumbele hivyo kama shirika wameona ipo haja ya kuja na mkakati wa kupunguza vifo vya majini kwa kuhakikisha wavuvi wanapoingia ziwani wawe na vifaa vya kujikinga na ajali hizo.
Ameeleza kuwa tayari wameanza mkakati wa kupunguza ajali hizo kwa kushirikiana na serikali kutoa elimu namna ya kujikinga na ajali hizo.
“Eneo hili la ajali za majini limesahaulika mara nyingi tunasikia au kuona elimu ikitolewa kuhusiana na usalama wa barabarani au takwimu za ajali barabarani lakini hili la ajali za majini hatujaona jitihada zozote zikichukuliwa kuhakikisha ajali hizo hazitokei,”ameeleza Lukanga.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Kupunguza ajali za kuzama majini kutoka shirika la EMEDO, Arthur Mugema,ameeleza kuwa ipo haja kwa serikali kushusha gharama na kuondoa ushuru kwenye bidhaa za uokoaji majini ili kutoa nafasi kwa wavuvi na wasafiri wa majini kununua bidhaa hizo ka bei ya kawaida.
Amesema bidhaa hizo kama jaketi la uokoaji (lifejacket) zinauzwa kwa bei ghali jambo ambalo wavuvi hushindwa kumudu kununua na wakati mwingine hununua ambazo hazina ubora.
Jaketi yenye ubora na salama huuzwa kati ya shilingi 40,000 hadi 50,000 kiasi ambacho ni kikubwa hasa kwa mvuvi mdogo.
Huku akieleza kuwa sababu nyingine inayochangia ajali hizo ni imani za kishirikina kwamba wengi wanaamini kwamba ajali nyingi husababishwa na uchawi.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi