November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

EJAT yaongeza kundi la habari za ushirika

Na Hadija Bagasha Tanga,

Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya tuzo za umahiri za uandishi wa habari Tanzania (EJAT) 2021 limetangaza kuongezwa kwa kundi moja la kushindaniwa na kufanya makundi yanayoshindaniwa kwa sasa kuwa 19.

Kuongezwa kwa kundi hilo linafuatia ombi la tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania (TCDC) ya kutaka kuwa na kundi ambalo litahusisha habari za vyama ushirika nchini ikiwa ni pamoja na shughuli za vyama za vyama vya ushirika.

Awali akizungumza na waandishi wa habari Jjijini Tanga kutoka Mikoa mbalimbali nchini kuhusu kuongezwa kwa kundi la Habari za Ushirika katika Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2021 Ofisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Paul Mallimbo alisema kundi lililoongezwa ni tuzo ya uandishi wa habari za ushirika, ambalo wakati wa mashindano lilitazamwa katika vigezo vile vile vinavyotumika kwenye makundi mengine.

“Tuzo hizo zilizinduliwa na makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Joseph Sinde Warioba wakati wa kilele cha tuzo za 2020, september 10 2021 zilizofanyika jijini Daresalaam, “Alibainisha Mallimbo.

Aidha alisema makundi mengine yanayoshindaniwa katika tuzo hizo ni tuzo ya uandishi wa habari za, uchumi, biashara na fedha,
Tuzo ya uandishi wa habari za michezo na utamaduni, tuzo ya uandishi wa habari za kilimo na biashara ya kilimo , tuzo za uandishi wa habari za elimu, tuzo ya, uandishi wa habari wa za utalii na uhifadhi, tuzo za uandishi wa habari za uchunguzi, na tuzo za uandishi wa habari za data.

Mallimbo alisema makundi mengine ni tuzo za uandishi wa habari za haki za, binadamu na utawala bora, mpiga picha bora-magazeti, mpiga picha bora-runinga, mchora katuni bora, tuzo ya uandishi wa habari za jinsia na watoto, tuzo ya uandishi wa habari za gesi, mafuta na uchimbaji madini, tuzo za uandishi wa habari walemavu, tuzo za uandishi wa habari za afya, tuzo za uandishi wa sayansi na teknolojia, tuzo za uandishi wa habari za hedhi salama, tuzo za uandishi w habari za ushirika na kumdi la wazi.

Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Henjewele John akizungumzia kundi hilo amesema kuwa amesema uwepo wa kundi hilo utasaidia kwa kiwango kikubwa jamii katika kutoa elimu ya masuala mbalimbali ikiwemo, kilimo na ufugaji sambamba na kutengeneza fursa za masoko kwa wakulima hususani katika sekta ya mifugo.

Hata hivyo kamati ya maandalizi ya EJAT inayoongozwa na baraza la habari Tanzania (MCT) na washirika wake ni pamoja na mfuko wa vyombo vya habari Tanzania (TMF), Taasisi ya Vyombo vya habari kusini mwa Afrika-tawi la Tanzania (MISA-TAN), chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Haki elimu, SIKIKA na umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC).

Kundi hilo lililoongezwa linakwenda kuongeza idadi ya makundi 18 yaliyokuwepo awali na kufanya sasa kuwa jumla ya makundi 19.