January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dula Makabila aamia rasmi Simba

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki miondoko ya Singeli hapa nchini Dulla Makabila, leo ameamua rasmi kuamia katika klabu ya Simba akitokea Yanga, baada ya kuona klabu hiyo ikifanya vyema huku klabu yake ya zamani ikienda kwa kusuasua katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu licha ya kuongoza Ligi.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Makabila amesema, halikuwa chaguo lake kuwa mshabiki wa YAnga lakini Marehemu Baba yake ndio alimshinikiza kupenda klabu hiyo.

”Kuna muda mnaweza kuniona mtu wa ajabu kwa sababu wimbo wangu wa kwanza ulionitoa kimziki nilikuwa nimewaimbia Yanga, lakini leo (jana), nimeahamia rasmi klabu ya Simba.

“Kiukweli Yanga halikuwa chaguo langu kabisa, ila miaka kadhaa huko nyuma Marehemu Baba yangu alifululiza kuninunulia Jezi za Yanga mpaka nakuwa mkubwa najikuta nipo Yanga. Samahanini sana mashabiki wa Yanga kwa yeyote niliyemkwaza kwa hili na poleni pia familia yangu, najua mtanitenga sababu nimehama timu ambayo Baba yangu mzazi alipenda kuona nashangilia.

“Mara nyingi kila nikitazama mechi yeyote ya Simba ikifungwa huwa naumia Sana, kiasi hata kukosa raha siku nzima. Hapo ndipo nilipogundua kwamba mimi ni shabiki halali wa Simba niliyelelewa na shabiki wa Yanga ambae ni Baba yangu Mzazi.

“Ndugu zangu hakuna asiyejua ‘Strees’ za Yanga, yaani Yanga hata wakisema kila mechi inapoisha wanampa kila shabiki milioni, sirudi na wala sina hilo wazo. Huo wimbo niliowaimbia Yanga nitafanya kama nimetoa Sadaka. Na naandaa wimbo kwaajiri ya Simba sasa. Asante sana msemaji wa Simba Haji Manara kwa mapokezi mazuri,” ameandika Makabila.