December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Doyo :Sitambui uchaguzi wa uongozi ADC

Na Penina Malundo, Timesmajira

ALIYEKUWA Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti kupitia Chama Cha Alliance For Democratic Change (ADC) Doyo Hassan Doyo amesema kuwa hautambui uchaguzi wa viongozi wa Chama hicho na kusisitiza kuwa ulienda kinyume na katiba na kanuni za Chama hicho.

Doyo ambaye katika uchaguzi huo alishindwa huku mpinzani wake Shabani Itutu akichukua nafasi hiyo amesisitiza kuwa Chama hicho kinapaswa kurudia uchaguzi huo upya ukiwa chini ya Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa.

Doyo ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam leo Julai 1,amesema hajaridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali hivyo amekata rufaa katika kamati ya uchaguzi ya Chama kama inavyoelekeza katika kanuni.

Akitaja sababu za kutokukubali uchaguzi huo Doyo amesema Mkutano huo wa uchaguzi ulikwenda kinyume na katiba na kanuni kutokana na kuongozwa na Mwenyekiti Mstaafu Hamad Rashid Mohammed jambo ambalo ni kinyume na katiba na kanuni.

“Mwenyekiti Mstaafu Hamadi Rashidi Mohamed aliongoza mkutano kimakosa hivyo alivunja kanuni zilizo kwenye katiba kwani katiba inasema Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utaongozo na Mwenyekiti wa muda atakayechaguliwa lakini haikuwa hivyo Mkutano ule uliongozwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hamadi Rashidi Mohamed hoja yetu ya rufaa tunahoji kateuliwa na nani kuendesha mkutano ule na hakukua na tamko lolote” amesema.

DoyoPia amesema kuwa tayari wamepeleka rufaa ya kupinga matokeo hayo kutokana na mkutano huo kuongozwa na Mwenyekiti muda ambaye anaeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Katiba ya chama.

“Mwenyekiti wa muda kwa mujibu wa kifungu hiki anatakiwa uchaguzi wa nafasi ya uchaguzi huo kitendo Cha Mwenyekiti anaemaliza muda wake Hamad Rashid mkutano mkuu wote Hadi chaguzi za makamu Mwenyekiti Kwa upande wa Bara na Zanzibar amevunja kanuni za Chama hivyo uchaguzi uchaguzi ni batili “ Amesema Doyo.

Aidha ameongeza kuwa taratibu za kupiga kura pia hazikuzingatiwa kwani wajumbe walikuwa wamezidi idadi inayotakiwa ambapo rejesta inayopelekwa kwa Msajili wa vyama vya siasa haikutumika kuongeza idadi ya kura za sheria 192 na kuwepo kwa kura 200.Sambamba na hayo amesema Viongozi wapya wengi waliochaguliwa ni ndugu Mwenyekiti anaemaliza muda wake Hamad Rashid ambao amechagua mwenyewe hivyo inadhihirisha kuwa anamaliza muda wake ila upande wa pili anakitaka Chama Kwa mgongo wa nyuma.

Hata hivyo Doyo amewashukuru Wapiga Kura 70 waliomwamini na kumpigia kura kati ya wajumbe halali 192 ambapo kwenye sanduku zilikutwa kura 200 ambapo kura hizo ni sawa na Kanda 7 kati ya 10.Kwa upande wake aliyekuwa Mgombea nafasi ya makamu mwenyekiti Zanzibar Shara Amrani Khamism amesema ajaridhishwa na namna uchaguzi ulivyofanyika kutokana na kuwa na chagamoto nyingi hivyo anaunga hoja zilizotolewa na Doyo.