Na Esther Macha, Timesmajira,Online ,Mbeya
SPIKA wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini , Dkt.Tulia Ackson amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kutoa taarifa za wananchi wenye changamoto ya chakula inayopelekea kulala na njaa na kutoa taarifa kwa watendaji wa Kata ili waweze kusaidiwa.
Dkt,Tulia alitoa agizo hilo jana mara baada ya kutoa kadi za bima ya afya ya Jamii iliyoboreshwa (ICHF ,) kwa wananchi 3,000 katika kaya 500 Jijini hapa kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust.
“Natambua katika maeneo yenu kuna changamoto nyingi kwenye jamii inayowazunguka hivyo nikiwa kama Mbunge wenu sipeni kuona kama kuna wananchi wanalala njaa kwa kukosa chakula ”,amesema.
Amesema kuwa majukumu ya viongozi wa Serikali za Mitaa ni kuangalia maisha ya wananchi mnaowaongoza ufike wakati taarifa za watu wenye changamoto kwenye maeneo yenu ziwe zinatolewa kwa wakati ili ziweze kutafutiwa ufumbiza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani katika kuboresha huduma kwa jamii.
Amesema kuwa katika utekelezaji ya ilani ya chama cha mapinduzi wanafanya kazi ya kusaidia wananchi waweze kupata matibabu vizuri kwa kuwa na vituo vya afya vya kutosha.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya , DourMohamed Issa amesema kuwa kama madiwani hawako tayari kupoteza jimbo la mbeya mjini kwani limepiga hatua kubwa katika maeneo mbali mbali ikiwemo afya , elimu , maji ,barabara.
Amesema kuwa uwepo wa Dkt. Tulia umesaidia kwa kiasi kubwa kuwaweka sawa na kuwaunganisha madiwani kwa pamoja katika kusimamia shughuli za maendeleo kwenye kata zao .
Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,Ayas Njalambaa amesema kuwa mkoa wa Mbeya umepata tunu ya kuwa na kiongozi anayefanya vizuri kwa kugusa nyanja mbalimbali hivyo ni jukumu letu wanambeya na watanzania kumuombea.
“Wanambeya kila mtu kwa imani yake tuwe mstari wa kumwombea kiongozi watu kwani hii ni Tunu hatutakiwa kuipoteza kabisa na tumuunge mkono anapofanya kazi za maendeleo ya mkoa wetu “amesema.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi