Na Esther Macha,TimesMajiraOnline, Mbeya
SPIKA wa bunge na Mbunge wa jimbo la Mbeya na Rais umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson amewezesha vijana 20 mkoani hapa kwa kuwapatia ajira baada ya kuhitimu mafunzo ya uanagenzi wa fani mbali mbali katika chuo cha Ufundi Ruanda kinachomilikiwa na Jeshi la magereza .
Mbali ya kuwapatia ajira vijana hao pia amewawezesha nauli kwa tiketi pamoja na fedha za kujikimu wakiwa safarini kuelekea mkoani Pwani ambako kitakuwa kituo chao cha kazi.
Akizungumza Mei 2 ,2024 kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini na Spika wa Bunge Katibu wa Mbunge ,Stephen Chambanenge amesema kuwa katika jitihada za kuwasaidia vijana hiyo ni awamu pili kuwapatia ajira vijana 40 na Dkt.Tulia ikiwa ni ahadi yake wakati wa kampeni katika kuwezesha vijana kiuchumi na kuwatafutia ajira.
Chambanenge amesema kuwa Dkt. Tulia ametoa msaada kwa vijana kuwatafutia fursa vijana ambao waliihitimu mafunzo ya fanui mbali mbali mwaka jana na kuishia mitaani kutokana na kukosa ajira na Mbunge akaamua kuwasaidia kupatia ajira.
“Mh.Mbunge amewatafutia fursa ya ajira kwa vijana ambao wamekuwa wakisoma chuo cha ufundi Ruanda Magereza kwa fani mbalimbali,na kusema kuna kiwanda kipo mkoani Pwani ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa vitu mbali mbali ambapo vijana kabla ya kumaliza walikuwa baada ya kuhitimu mafunzo hayo vijana hawakuwa na ajira kutokana na juhudi za Dkt.Tulia lazima vijana wa mbeya mjini wapate ajira na amefanya kazi ya ziada kupata sehemu ambako vijana watafanya kazi kwa mwaka mmoja na wengine watakaofanya kazi vizuri zaidi watapata mkataba wa kudumu lakini kwasasa watapata mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja,niwaombe vijana wa Mbeya mjini kujiunga na chuo hiki ili kuweza kupata fursa ya kutafutiwa ajira kwani ajira zinazotangazwa na serikali zinajumuisha watu wangu ambao wachache wanaopata asilimia kubwa wanabaki mtaani.
Aidha Katibu huyo Mbunge amesema kuwa Dkt.Tulia anaungana na serikali kuwapatia ajira vijana na Mbunge huyo kutafuta namna nyingine ya kuwasaidia vijana na kusema kiongozi huyo ni mtu wa kujiongeza kwa kuwatafutia ajira vijana ,kupitia mitaji na shughuli mbali mbali na bado amekuwa hachoki kwa kuangalia nje ya mkoa wa Mbeya kuweza kuwatafutia ajira na kusema Mh. Mbunge atahakikisha mpango huo unaendelea na kuwa kama tawi ili vijana wengine waweze kupata ajira.
“Mh. Mbunge amehakikisha vijana wanaoenda mkoani Pwani kufanya kazi ni kuwa vijana wote 20 wanapatiwa nauli kwa kukabidhiwa tiketi ya kutoka Mbeya mpaka Kibaha lakini pia wamekabidhiwa fedha za kujikimu wakiwa safarini na bado ofisi ya Mbunge itahakikisha vijana wanasafiri salama pamoja na kupolewa salama kwasasabu taarifa ya vijana hao itaendelea kufuatiliwa na Ofisi ya Mbunge “amesema Katibu wa Mbunge Chambanenge.
Kwa upande wake mkufunzi mkuu wa chuo cha Ufundi Magereza Ruanda ,Asumin Mbunda ameshukuru kwa msaada huo wa kuwapatia vijana ajira na kusema kuwa awamu hii ni ya pili kwa vijana kupatiwa ajira na kuwa kwa taarifa vijana 40 waliopelekwa awamu ya kwanza wanaendelea kufanya vizuri.
“Nawaombeni vijana kutunza nidhamu yenu mtafanikiwa vizuri kazi mtakazopewa mkafanye kwa utulivu mzuri ili muweze kufika mbali ,bado tuna uhitaji wa hizi nafasi hivyo kubwa ni kutunza heshima yenu mliyojifunza hapa chuoni kwa muda wote mliokuwa mnasoma hapa ikiwa ni pamoja na kushirikiana ”amesema.
Rehema Joseph ni Mhitimu wa fani ya fundi bomba katika chuo cha Ufundi Ruanda Magereza amemshukuru Mbunge jimbo la Mbeya kwa fursa waliyopatiwa kwani baada ya kumaliza mafunzo mwaka jana walikuwa mtaani tu na kusema watakuwa mabarozi wazuri ili kuwa mfano kwa wengine .
Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu imekuwa ikitekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi kwa njia mbali mbali ikiwemo uanagenzi, mafunzo ya vitendo mahali pa kazi na utambuzi wa ujuzi uliyopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo.
Mitindo ya Mavazi na Ushonaji, Ufundi Bomba, Useremala, Uchomeleaji Vyuma, Uchongaji wa Vipuri vya Mitambo, Uashi, Uwekaji waTerrazo na Vigae kwenye majengo, Ufundi Magari na Mitambo, Kilimo na Ufugaji, Kutengeza Komputa.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi