Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
SPIKA wa bunge na Mbunge wa jimbo la mbeya mjini Dkt. Tulia Aksonamekea vikali tabia ya baadhi ya watu wanaobeza kazi za maendeleo zinazofanywa na viongozi wa kitaifa kwa kuona kuwa hakuna chochote wanachofanya.
Dkt Tulia amesema hayo jana wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM)Wilaya ya mbeya Mjini kwakipindi cha mwaka 2021/2022 kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalum wachama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Tughimbe Jijini hapa.
Dkt .Tulia amesema kuwa kuna baadhi ya watu wasiopenda maendeleowanapoona viongozi wakiwemo wa kitaifa wakifanya kazi nzuri kwajamii hubeza na kupambana na majungu kwa kukosoa utendaji ilikuleta mkanganyiko usio na faifa kwa wananchi .
Hata hivyo Dkt.Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini amewatakawananchi wakiwemo wa jimbo hilo kuendelea kumuunga mkono katikamajukumu yake ili aweze kuwatimizia mahitaji mahitaji yao ikiwemo uborreshaji miundo mbinu elimu , afya kwa kushirikiana na serikaliya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia suluhu Hassan.
“Ndani ya chama hiki tunahitaji wadau njooni tuwaonyeshe eneo mjengeukumbi mzuri ndani ya chama tunaheshimiana ndo maana demokrasia yakeni pana anasikilizwa kila kwenye kikao nafasi za kugombea kila mtu,wala msiwe na wasiwasi fursa zinazotolewa zipo wazi kwa kila mtuchama hiki kina maeneo mengi yapo wazi na tutakusema hadharani kuwaumetujengea ukumbi mzuri kwa shilingi 20,000 yako , chama kinamuheshimu kila mtu hivyo tuheshimiane sasa ni muda wa kazi na nafasi ambazo hazijajazwa tunasubiri wajae ili CCM iweze kusonga mbele mtummoja asitake kukivuruga chama hiki kitaendelea kusimama , weweusiwepo chama kitazidi kusonga mbele walikuwepo na wakaondoka nachama kikasonga mbele “amesema Dkt.Tulia.
Dkt.Tulia amesema hayo kufuatia watu wanaoibuka kubeza ukumbi waDkt.Tulia uliojengwa na spika kwa kudai ukumbi huo ni darasakutokana na kujengwa kwa fedha ndogo ambayo ni mil.20 , weweunayebisha njoo uje ujenge maeneo yapo mengi tukuonyeshe eneoukatumia hiyo mil.20 kujenga huo ukumbi .
Humprey Nsomba ni Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbeyamjini (CCM) amesema kuwa amemtaka Dkt. Tulia kutokata tama kazianazofanya bali asonge mbele zaidi na asirudi nyumba .
“Kama unabeza kazi iliyofanywa na Mbunge wetu tukuweke kwenye kundigani ukumbi ule kabla ya kukamilika ulikuwa kama pagala leo hii mtuanajitokeza kubeza ujenzi wa ukumbi ule , ndo maana wana mbeya huwatunaenda mbele na kurudi nyuma tumepata kiongozi ambaye amesimamaanafanya mambo kwa uhakika badala ya kumtia nguvu na kumpa moyoaendelee kutufanyia mambo mengi tunabaki kumkatisha tamaa “amesemamwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Naibu waziri wa maji na Mbunge wa vitimaalum mkoa waMbeya , Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa Mbeya ni mkoa wenye jina kubwa sana lakini kimaendeleo bado kuna mikoa haina jina kubwakama mbeya lakini mambo yao yapo vizuri mnoo.
Mhandisi Mahundi amesema kuwa kumekuwa na maneno ya kumizana sanaambayo ndo inatufanya tusifike mbali hivyo kufikia hatua yakukatishana tamaa , viongozi wengib hatuna muda hata wa kukaa nafamilia , sisi watu Mbeya tukimtumia vizuri Dkt. Tulia tutawaka sanatumpe ushirikiano mbunge wetu aweze kufika mbali zaidi katikautekelezaji wa shughuli za maendeleo .
“Naomba tumpe raha Dkt. Tulia aweze kutuhudumia zaidi na zaidi katikakutekeleza shughuli zote za maendeleo ili chama chetu kiweze kusongambele” amesema mhandisi Mahundi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba