Na Esther Macha,Timesmajira,Online,Mbeya
MBUNGE wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano Tanzania,Dkt.Tulia Akson amewataka madiwani waliokula kiapo kwenda kuwatukia wananchi kwa kuwasilisha kero zao kwenye vikao vya mabaraza na si kuwasilisha mawazo yao Binafsi.
Dkt,Tulia amewaeleza leo kwenye kikao cha kwanza cha baraza la madiwani sambamba na kura kiapo Cha uadilifu na kufanya uchaguzi wa Mstahiki Meya na Naibu Meya wa Jiji la Mbeya kilichofanya katika ukumbi wa Mkapa.
Amesema madiwani hao wanapaswa kuweka hoja za wananchi na sio hoja zao binafsi kuzipa kipaumbele hivyo wanatakiwa kuleta maendeleo katika kata zao.
Dkt.Tulia amesema kuwa kila diwani anatakiwa kujua wajibu wake wa kuwasikiliza wananchi wao ili kuweza kuwaletea maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya,Paul Ntika amesema kuwa kwasasa mbeya inapendeza hivyo madiwani waliochaguliwa watoe ushirikiano katika suala zima la shughuli za maendeleo la Jiji hilo.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa meya na naibu meya Msimamizi wa uchaguzi huo ,Saitot Zelothe amewatangaza Agnes Mangasira kuwa Naibu Meya wa jiji la Mbeya kwa kupata kura 46 ,huku Meya wa Jiji la mbeya akitangazwa kuwa DorMohamed Issa ambaye alipata kura 47.
More Stories
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa