December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Tulia ashiriki ufunguzi mkutano wa masuala ya usalama

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

RAIS wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mei 20,2024 ameshiriki Ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Nyuklia (ICONS-2024) unaofanyika Vienna nchini Austria.

Dkt. Tulia akiwakilisha IPU kwenye Mkutano huo, ameshiriki pamoja na Wajumbe wengine kujadili kuhusu Usalama wa Nyuklia na jukumu la Nchi zote kuhuhisha Mkataba wa Kimataifa wa Matumizi Salama ya Nyuklia katika ngazi za ndani za Mataifa yao.