January 26, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Tulia akabidhi msaada wa bati bando tano kata ya Iyela

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

TAASISI ya Tulia Trust inayoongozwa na Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt Tulia Ackson imekabidhi msaada wa bati bando tisa kwa kata ya Iyela kwa ajili ya kusaidia kuezeka ukumbi wa mikutano wa barozi shina namba 8.

Akikabidhi msaada huo Julai 3,2024 kwa niaba ya Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Katibu wa Mbunge, Stephen Chambanenge amesema msaada huo wa bati ni ahadi aliyoitoa hivi karibuni Dkt Tulia katika moja ya mikutano yake ya hadhara ambayo amefanya ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo Jijini hapa .

“Nimekuja kukabidhi bati bando tano ambazo nimetumwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Dkt.Tulia Ackson kama mlivyoomba ili ziweze kusaidia kuezeka ukumbi huu wa mikutano ambao naamini utatumika kwa shughuli nyingi katika kata hii hususani barozi shina 8 na majirani zenu “amesema Chambanenge.

Hata hivyo Chambanenge amesema pia kata hiyo itaongoza katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Mwezi Novemba mwaka huu,na kusema kuwa kwa upande wa mwakani shughuli imekwisha kwa upande wa Rais ambapo hawahitaji kuongea na upande wa Mbunge hawahitaji kuongea kama ni uchaguzi ndani ya chama umeisha na hata wale wanaohitaji kuchukua fomu wachukue ili warudi na sifuri nyumbani .

Aidha Chambanenge amesema kuwa wana CCM Wanajua hitaji la moyo kwani wanaona maendeleo yanayofanyika katika kata ya Iyela ikiwemo vituo vya afya,barabara pamoja na miundombinu ya shule.

Kwa upande wake Barozi ya shina namba 8 kata y Iyela ,Gaporicr Lwiba amesema kuwa ukumbi huo si kwa ajili barozi shina namba 8 ni kwa ajili ya Jamii ya wana Iyela.

Amesema kuwa pia wataribisha barozi zingine kufanya mikutano ya kijamii na nyakati za asubuhi kufundishia watoto wa chekechea pamoja kukodisha ukumbi ili fedha itakayopatikana iweze kufanya shughuli mbalimbali za kichama na kiserikali.

Mkazi mwingine wa Kata ya Iyela ,lusako msopole amemshukuru DKT.Tullia kwa msaada huo wa bati na kuhaidi kuzitunza na kusema hakuna kipande kitakachopotea au kuibwa wakati ujenzi unaendelea.