Na Penina Malundo,timesmajira, Online
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amewataka wanachama na watendaji wote wa Chama cha CCM kwenda na kasi ya mabadiliko.
Dk. Shein aliyasema hayo leo katika sherehe ya uzinduzi wa maadhimisho hayo iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwehe, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali waandamizi wa Chama na serikali.
Amesema miaka 45 ya CCM imeleta mafanikio makubwa ikiwamo, ni vyema kuyalinda, kuyaendeleza na kuhakikisha nchi ina inafika mbali kimaendeleo.
“Miaka ya CCM imeacha maendeleo makubwa ya kupigiwa mfano nchini na Afrika kwa ujumla…katika ulimwengu huu ni vyema kuongeza katika kazi na kuacha utendaji wa mazoea ili kujiletea tija na maendeleo zaidi,” amesema.
Dk. Shein ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, amewataka watumishi ndani ya CCM na serikali kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mabadiliko ikiwamo kujitegemea.
Awali akiwasilisha salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdallah, amesema serikali inaendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi kama ilivyoelekezwa na Chama.
Naye Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwasilisha salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema wataendelea kutekeleza kwa upelekeaji maendeleo kwa wananchi.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua