Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MKURUGENZI Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO)Kanda ya Afrika Dkt.Faustine Ndungulile, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni amesema mwaka 2025 mwezi February anatarajia kuanza kazi rasmi WHO hivyo atajivua nafasi ya Ubunge wa Kigamboni .
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani WHO Dkt. Faustine Ndungulile, alisema hayo wakati wa Mapokezi yake leo Agosti 31 saa tisa usiku alipowasili na Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Teminal 2 jengo la VIP, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
“Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ,kwa kupendekeza jina langu katika wadhifa huu mkubwa wa cheo cha Mkurugenzi wa shirika la Afya kanda ya Afrika ushindi wangu heshima kwa Tanzania kwa sasa nakuwa Msimamizi Mkuu katika Bara la Afrika” alisema Dkt. Ndungulile.
Dkt ,Ndungulile alisema katika kinyanganyiro hicho wagombea walikuwa 47 kugombea nafasi ya utendaji Mwenyezi Mungu amebariki na ameweza kushinda uchaguzi huo watanzania wamesali na kumuombea dua katika kinyanganyiro hicho.
Dkt.Faustine Ndungulile alisema anaenda kuongeza nguvu katika shirika hilo uzoefu anao akiwa Mbunge na Waziri ataenda Simamia vizuri shirika hilo.
Katika mapokezi hayo yaliofanyika usiku alipokelewa na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Amana pamoja na Watumishi wa WHO , Familia yake na Dkt Grace Magembe.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â