December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Nchimbi amalizana na Singida sasa zamu ya Manyara

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Singida

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi akizungumza na Wananchi wa Kata ya Itaja, Jimbo la Singida Kaskazini, wakati akiwa njiani kuelekea Manyara ikiwa ni katika muendelezo wa ziara yake ya mikoa mitano.

Ziara ya Dkt Nchimbi inalenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo ipo ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/2024 pamoja na kuzungumza na makundi mbalimbali ya Kijamii.

Kupitia ziara hiyo Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA. Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC, Mambo ya Siasa na uhusiano wa Kimataifa, Rabia Hamid.