Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya
MKUU wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki(KKAM) Askofu Oscar John Ulotu amemsimika rasmi Askofu Dkt. Edward Mwaikali kuwa Askofu wa Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini.
Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Ottu Jijini Mbeya na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera sambamba na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amempongeza Dkt Mwaikali kwa uvumilivu katika kipindi chote cha mgogoro na kwamba serikali ipo pamoja naye zaidi akimtaka kuhubiri injili.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei ameshukuru kuwepo kwa amani kipindi cha mgogoro na kwamba atachangia pindi watakapoanza ujenzi.
Wakuu wa Jimbo watatu wachungaji zaidi ya arobani na wainjilisti zaidi ya mia wamejiondoa KKKT Dayosisi ya Konde na kujiunga na KKAM Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini.
Wakili Mussa Mwapongo amekabidhi ekari 45 eneo la Mpemba na Shule ya Chekechea na katika hatua nyingine muumini mwingine amekabidhi ekari mbili kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa Parish ya Ruanda.
Harambee kwa ajili ya gari la Askofu Dkt Mwaikali zimepatikana zaidi ya 8m.
Askofu Mwaikali amekabidhiwa vitendea kazi kama kiti,fimbo,katiba na muongozo wa Dkt Martin Luther vilivyokabidhiwa na katibu wa kanisa hilo nchini Heroic Moses Mkwizu.
More Stories
The Desk & Chair yashusha neema Gereza la Butimba
TVLA,yapongezwa kwa kuzalisha chanjo
TAKUKURU,yasaidia kurejesha hekali 8