November 14, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Mataragio:Gesi iliyogunduliwa hadi sasa futi za ujazo 57.5


Na Mwandishi wetu, timesmajira, Online
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio amesema kuwa kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa mpaka sasa ni futi za ujazo Trilioni 57.5 huku kiasi kikubwa kikiwa baharini.
Ameyasema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara maarufu sabasaba yanayoendelea kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Dk. Mataragio amesema kiasi kikubwa cha gesi ambacho kipo baharini kinatarajiwa kuvunwa kupitia mtambo wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) ambapo  unaotarajiwa kujengwa nchini.
“Hatua ambayo tumefikia mpaka sasa katika ujenzi wa mtandao  huo wa LNG, ni makubaliano ya awali yamefanyika, lengo letu itakapofika Desemba tuwe tumemaliza kukubaliana mambo yote na kuingia katika hatua nyingine za kiuhandisi,” amesema
Amesema asilimia 62 ya umeme nchini unazalishwa na gesi asilia huku kiasi kinachobakia  asilimia 20 kinatumika katika maeneo ya majumbani na kwenye magari.
“Tuna mpango wa kujenga vituo vitano vya gesi ambavyo vitakuwa katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Feri, Muhimbili, Kibaha na Ubungo, vituo hivi tunategemea vitakamilika mwakani mwezi Machi vitakuwa ni moja ya vichocheo vya upatikanaji wa gesi asilia katika magari na majumbani,” amesema
Aidha  amezitaka sekta binafsi kujitokeza kwa wingi kujenga vituo vidogo vidogo vya gesi asilia ili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa wananchi.
Mmmmwishoooo