January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Mahela :Serikali yaanza kutekeleza mpango ufundishaji elimu kwa vitendo

Na Stephen Noel ,Mpwapwa


Naibu katibu Mkuu wizara ya Elimu sayansi na Teknolijia Dkt Charles Mahela amesema ili kuweza kuondoa changamoto ya Ajira Kwa vijana hasa wanao maliza vyuo serikali imeanza kutekeleza mpango ufundishaji mtaala wa Elimu ya amali (Elimu Kwa Vitendo)

Ameyasema hayo wilayani Mpwapwa Katika hafla ya kukabithi vitabu 2835 vya kiada na ziada Katika chuo cha ualimu Mpwapwa .

Amesema ili kuweza kuwa na Taifa imara lazima waweze kuweza Katika sekta Elimu kwa kuimarisha Miundo Mbinu ya kujifunzia na kufundishia ikiwa sambamba na kushughulikia changamoto mbalimbali za walimu ikiwemo mapunjo na madai mbalimbali.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho, Gerard Richard amesema kwa sasa chuo cha ualimu Mpwapwa ni miongoni mwa vyuo vinavyotoa Elimu maluum kwa ngazi stashahada ili kuweza kupunguza changamoto ya walimu wa elimu maalum katika shule za msingi na sekondari ili kuweza kuwezesha upatikanaji wa Elimu jumuishi.

Aidha alidai kuwa kwa Sasa chuo hicho ni chuo kikokwe hapa nchini ambacho kilijengwa mwaka 1926 hivyo kutokana na ukongwe huo baadhi ya miundo Mbinu imechakaa na onahitaji ukarabati mkubwa na miundo Mbinu mengine inahitaji kujengwa upya.

Hata hivyo amesema chuo hicho chenye ambacho kinaweza kuwatunza wanachuo wapatao 1200 ambacho kwa sasa kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa bwalo la chakula ambalo husababisha wanachuo wengi kulia nje kitu alichosema kipindi cha mvua kinakuwa na usumbufu mkubwa kwa wananchuo.