Na Penina Malundo, timesmajira Online
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dk. Khatibu Kazungu, amewataka wadau mbalimbali wa Asasi za Kiraia kutoa maoni yao juu ya maboresho ya rasimu ya mpango kazi wa pili wa taifa wa haki za binadamu nchini (2021-2026).
Akitoa wito huo leo jijini Dar es Salaam , Dkt.Kazungu katika kikao cha wadau wa haki za binadamu kwa ajili ya kuhakiki rasimu hiyo.
Amesema ni matarajio yake kuona wadau hao wataweza kuwasilisha michango yao juu ya namna ya kuboresha rasimi ya mpango kazi.” Naamini baada ya kupitia rasimu iliyopo mtatoa michango yenu kikamilify kwa kuwa mchakato unaendelea zoezi hili ni muhimu kuhakikisha Serikali inakamilisha wajibu wake wa kukuza na kulinda haki za binadamu,” amesema Dk. Kazungu,”
Dk. Kazungu amesema rasimu hiyo imezingatia masuala mbalimbali yanayohusu haki za binadamu na watu Tanzania, ikiwemo haki za kiraia na kisiasa, haki za kiuchumi na utamaduni na haki za makundi maalumu.
“Moja ya haki ya kiraia na kisiasa, yafuatayo yamezingatiwa ikiwemo upatikanaji wa haki na usawa mbele ya sheria, uhuru wa mawazo na kujieleza na kuoata taarifa. Kwenye haki za kiuchumi, utamaduni na kijamii, imezingatua haki ya kuoata maendeleo na kuishi kwenye mazingira safi na salama,” amesema Dk. Kazungu.
Kwa upande wake Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema asasi za kiraia zitaendelea kutoa ushirikiano wake kwa Serikali, katika uimarishaji haki za binadamu.
“Mchakato huu unazingatia hatua tano,hatua ya kuoata maoni na uandaaji, ufuatiliaji, utekelezaji na hatua ya kufanya tathimini na yote hii asasi tumekuwa wadau wanaosimamia utekelezaji haki hizo. Asasi tupo pamoja na Serikalo yetu na tutaendleea kuendeleza ushirkiano,” amesema Olengurumwa.
Kikao hicho kimeandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), na kuhudhuriwa na wanachama kutoka asasi za kiraia mbalimbali.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa