Na Mwandishi wetu, Timesmajira
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima amesema Serikali wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuweka msingi unaochochea mabadiliko yanayojielekeza kukua kiuchumi.
Â
Hatua hii ya serikali inakuja wakati ambapo tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa bado kuna kundi kubwa la watu ambao bado hawajafikiwa na huduma za kifedha ambapo kwa asilimia kubwa wengi ambao hawajafikiwa ni wanawake hali hiyo ikitokana na kukosa elimu juu ya umuhimu wa kutumia huduma za kifedha.
Waziri Dkt Gwajima ametoa kauli hiyo Jijini Dar Es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa Dirisha maalum ya wanawake la Benki ya Equity , Mwanamke Plus ambayo ina lengo la kumkomboa mwanamke.
Waziri Gwajima amesema Sera ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ni ya muhimu katika kukuza usawa wa kijinsia hasa kutokana na kuweka kipambele kwa ushiriki wa wanaume katika jitihada za kujenga usawa wa kijinsia na kutoa wito kwa benki hiyo kubuni na kutoa bidhaa za kifedha kwa kundi ka wanaume ili nao wasiwe nyuma kiuchumi.
Â
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Isabela Maganga amesema benki hiyo ina lengo la kuhakikisha kuwa fedha za wanawake wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo zinapita katika mfumo rasmi ya kibenki ili kuweza kusaidia wafanyabiashara kukuza biashara zao.
Kupitia Mwananke Plus wanawake wote watafikiwa na kupewa elimu juu ya fedha na namna gani wataweza kukuza mitaji yao kupitia fursa mbalimbali zitolewazi na benki hiyo kama vile mikiopo.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba