Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makumdi Maalumu Dkt. Zainab Chaula amewataka Wahitimu 31 wa Kozi ya Utabibu katika Chuo cha Afya cha Padre Pio College of Health and Allied Science, kuhakikisha Wanatumia Elimu waliyopata inakuwa na Manufaa kwa Jamii watakayo kwenda kuhimdumia.
Dkt.Chaula ameto wito huo leo Februari 24, 2023 Wakati wa Mahafali ya pili ya Chuo hicho kinachotoa kozi za Masuala ya Afya.
Mahafali hayo ya pili yamekwenda sambamba za Uzinduzi wa Dawati la Jinsia Chuoni hapo, ambapo amewasisitiza kutumia Dawati hilo ipasavyo ili kukomesha kabisa Vitendo vya Ukatili kwenye Chuo hicho.
Uendeshaji na ufuatiliaji wa Dawati la Jinsia ulizinduliwa na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 25 Novemba, 2021, wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia uliofanyika Mkoani Dar es salaam.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi