Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula,ametoa rai kwa wasanii wa wilayani Ilemela mkoani Mwanza,kutumia ujuzi wao kuelimisha na kukemea maovu katika jamii.
Dkt.Angeline ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wasanii hao,katika tamasha la wasanii wa Wilaya ya Ilemela,lililofanyika Februari 19,mwaka huu uwanja wa CCM Kirumba wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Ambapo ameeleza kuwa,zamani nyimbo na filamu zilikuwa zinalenga kuelimisha jamii hivyo wasanii hao wanaojishughulisha na vitu mbalimbali watumie ujuzi wao na kuuelekeza kwenye kuelimisha,kukemea maovu na kuhamisha jamii iwe wa moja.
“Watanzania ni wa moja,nanikisiwa cha amani watu wanakuja kujifunza hapa,tumieni filamu,kalamu zetu,utamaduni wetu kama zitakuwa na maudhui yanayojenga umoja,ukiangalia nyimbo za zamani pamoja na filamu nyingi zilikuwa zinalenga kuelimisha jamii,”.
Sanjari na hayo ameahidi kutoa Kuwapatia laptop kwa ajili ya wasanii hao kufanyia shughuli zao za uzalishaji pamoja na pikipiki kwa ajili ya usafiri.
Aidha amewashauri wasanii hao ili waweze kupata fursa mbalimbali za kiuchumi na serikali iwatambue warasimishe shughuli wanazofanya.
Pia ameeleza kuwa serikali imetenga kiasi cha zaidi ya bilioni 2 kwa ajili ya wasanii hivyo jukumu lao ni kuandika andiko vizuri na lieleze vitu watakavyoenda kufanya na namna watakavyo rejesha.
“Rasilimisheni shughuli zenu au biashara mnazozifanya ili muweze kufanikiwa lakini pia mjiunge katika shirikisho na bodi ya filamu itawatambua na kuwakopesha fedha kutoka kwenye mfuko wa Sanaa hivyo mtapata mitaji,”
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Waigizaji (TDFAA),Wilaya ya Ilemela,Malamala Shunashu,chama hicho kina jumla ya vikundi 54-58 katika Kata 19 za Wilaya ya Ilemela huku changamoto walizonazo ikiwa ni pamoja na kutokuwa na ofisi ya chama,vifaa vya uendeshaji na uzalishaji wa filamu.
Uhaba wa wataalamu wa kuandaa na kuzalisha filamu ikiwa ni pamoja na waongozaji wa filamu, waandishi wa miswaada, wataalamu wa urembo wa Sanaa, wataalamu wa picha na maandalizi ya uzalishaji kabla,wakati na baada.
“Changamoto za kiuchumi ambapo wasanii na wadau wote inatuwia vigimu kufanya uzalishaji wa filamu,warsha,mikutano,makongamano,seminar,mafunzo na kukutana na wadau wakongwe na wazoefu katika tasnia hii,kwa ajili ya kubadilisha uzoefu kwani hata yote yamekuwa yakifanyika mkoani Dar-es-Salaam na kwingineko na siyo Mwanza,”.
Hivyo ametoa ombi la kuwezeshwa kupata wataalamu na wakufunzi wa sanaa ya maigizo kutoka vyuo vya sanaa,kwa ajili ya mafunzo angalau mara mbili au zaidi kwa mwaka pamoja na kuwezeshwa kuoata ofisi ya chama na vifaa vya uzalishaji wa filamu.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato