Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Kufuatia changamoto ya maji katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Ilemela na Jiji la Mwanza kwa ujumla, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt. Angeline Mabula ametoa ufafanuzi juu ya jambo hilo.
Ambapo ameeleza sababu zinazochangia maji kuwa ni ya kusuasua katika maeneo hayo ni pamoja na miundombinu, kuharibika kwa moter pamoja na uzalishaji wa maji kuwa mdogo ukilinganisha na uhitaji ambao unasababishwa na ongezeko la watu.
Dkt.Angeline ametoa ufafanuzi huo baada ya kuibuka malalamiko kutoka kwa viongozi wa dini wakati wa majadiliano ya kimaendeleo jimboni Ilemela kupitia mafunzo ya uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022 na mapambano dhidi ya ukatili, kilichofanyika jimboni humo.
Ameeleza kuwa,tatizo kubwa lililopo ni miundombinu walinayo,ubovu uliojitokeza lakini pia chanzo cha maji kuwa na uzalishaji mdogo tofauti na mahitaji ya sasa.
Hivyo ameeleza kuwa kabla ya kuja katika kikao hicho amejiridhisha na tatizo kubwa ambalo lipo kwenye eneo la Mwanza,ni kuwa uwezo miundombinu ya uzalishaji wa maji ni changamoto huku akitolea mfano kuwa wanavyoongea hivi sasa uhitaji wa maji kwa siku ni lita za maji milioni 160 na yanayozalishwa ni lita milioni 90 hivyo Kuna upungufu wa lita za maji milioni 70.
Changamoto ya pili ni hivi karibuni mashine (moter) mbili za kusukumia maji ziliungua kwa pamoja na hawakupata mtu wa kutengeneza kwa hapa Mwanza hivyo walizipeleka Dar-es-Salaam pia walichofanya ni kuagiza moter nyingine mpya nje ya nchi ambazo nazo bado hazijafika.
Pia ameeleza kuwa,Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mwanza(MWAUWASA)walichofanya mpaka sasa wameandika mradi ambao tayari umeisha fikishwa Wizara ya Maji na umeishapelekwa Wizara ya Fedha,ili waone wanawezaje kutatua tatizo la maji.Aidha ameeleza kuwa amekuwa akipokea ujumbe
“kuwa sisi tuna Ziwa Victoria lakini tunakosa maji,maji yanaenda Igunga mnatutendea haki” huku changamoto iliopo sasa hivi ni miundombinu iliopo na ongezeko la idadi ya watu haliwezi kutatuliwa kwa siku moja.
“Nalijua tatizo lililopo lakini kwa maelezo ya Mkurugenzi MWAUWASA pia nimeliona andiko la mradi na ninamsubilia Waziri aje nimpeleke kwa wananchi aone kwamba kilio kipo na ni halisia,kwaio hapa kikubwa ni ule mradi wa maji Butimba ambao ukiisha lakini bado nao utakuwa hautoshelezi kwa sababu tuna upungufu wa maji lita milioni 70 na chanzo cha maji Butimba kitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 48, nao utakuwa hautoshelezi hivyo wameandika andiko jingine la ujenzi wa chanzo kingine cha maji Kabangaja,”ameeleza Dkt Angeline na kuongeza kuwa
“Chanzo hicho cha Butimba kikikamilika yale maji ya chanzo cha Capripoint watayafunga yaende upande mmoja ili yale ya Butimba,yagawe usawa huo mwingine wa kwenda Kisesa ukweli ni kwamba tutaendelea kutumia hizi mbinu ili kutatua changamoto ya maji,”.
Awali wakitoa kilio chao mbele ya Waziri huyo, viongozi wa dini pamoja na Mkurugenzi wa shirika la Kivulini Yassin Ali,ameeleza kuwa kilio chao kikubwa ni maji na ni jambo ambalo linewaumiza sana huku wakiohoji kuwa kukosa maji pia ni jambo la kikatili.
“Mbunge wetu,suala la maji suala la maji ni changamoto,halafu tunaziwa lakini kwenye mini yetu hatuna maji,Manispaa ya Ilemela hakuna maji,maji yauzwa,hainiingii akilini,”ameeleza Yassin.
Hata hivyo hivi karibuni Ofisa Uhusiano wa MWAUWASA Mohamed Saif,alieleza hali ya huduma ya maji katika maeneo ya pembezoni na ya milimani kwa kueleza kuwa kutokana na hitilafu ndogo kwenye mitambo yao ya kusukuma maji uzalishaji wa maji umepungua.
“Uzalishaji wetu wa maji umepungua kidogo na hivyo kusababisha upungufu wa maji hasa kwenye maeneo ya pembezoni pamoja na maeneo yenye miinuko (milimani),jitihada kubwa zinafanyika ili kuhakikisha tunarejesha huduma katika hali yake ya kawaida, katika kipindi hiki tulichonacho sasa, tunawaomba na kuwasihi wateja wetu kuhifadhi maji kila yanapotoka ili kuepuka usumbufu,”ameeleza Saif.
More Stories
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM