December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Abbas asisitiza kasi utekelezaji wa mradi REGROW

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas ameendesha Kikao Maalum cha Kamati ya Uongozi Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii (REGROW) kwa lengo la kupata uwelewa wa pamoja juu ya hatua mbalimbali zilizofikiwa za utekelezaji wa mradi kwa mwaka 2023/2024 na hatua za utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Katika kikao hicho Dkt. Abbas licha ya kupongeza jitihada mbalimbali zilifanywa katika utekelezaji wa mradi, ameagiza Taasisi zote zinazotekeleza Mradi kusimamia kikamilifu kazi zinazoendelea hususani Ujenzi wa miundombinu ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na si vinginevyo.

Dkt. Abbas amesisitiza kuwa, utekelezaji wa mradi wa REGROW ni mkakati madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuwaletea maendeleo wananchi kupitia sekta ya utalii, hivyo utekelezaji wake ni lazima uwendane na kasi ya Rais Samia kuwainua wananchi kiuchumi.

Kikao hicho kikichofanyika Jijini Dodoma, kimeudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara ya Maji, Wizara Kilimo, Wizara ya Fedha, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Wizara ya Maliasili ambaye ndio inatekeleza mradi huo.