Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
DIWANI wa Viti Maalum Wilaya ya Ilala Moza Mwano, amemsaidia Baskeli ya magurudumu mawili mwanafunzi Yasimin Ally (13)wa Shule ya Msingi Magore kata ya Mzinga ambaye ni Mlemavu ili aweze kutumia kwa ajili ya kwendea shule kusoma.
Diwani Moza Mwano alitoa msaada huo shuleni hapo mara baada kupata taarifa katika shule hiyo kuna mwanafunzi wa mwenye Ulemavu anapata shida kwenda shule kusoma.
“Leo nimekabidhi Baskeli mwanafunzi Yasimini atakuwa anatumia shule kwa ajili kusoma na kutembelea niliwezeshwa na wadau wangu ili mwanafunzi huyu naye awe na amani kama wezake aweze kupata elimu bora “alisema Moza.
Diwani Moza alisema yeye ni Diwani wa Viti Maalum wilaya ya Ilala yenye kata 36 ambapo anashirikiana na madiwani wenzake katika kutatua changamoto mbalimbali kwa ajili ya kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Diwani Moza alisema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Elimu amewekeza shule nyingi za msingi na Sekondari ambapo wao madiwani wa Halmashauri wanazisimamia na kutatua changamoto mbalimbali kuakikisha sekta ya elimu inakuwa wanafunzi waweze kufaulu.
Baba mzazi wa Yasimin Ally Yasini alimshukuru Diwani wa viti Maalum kwa kumuwezesha mwanawe aweze kusoma shule katika mazingira bora awe kama wanafunzi wezake awali mtoto wake alikuwa na changamoto kubwa kutokana na kukosa baskeli.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa