Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
DIWANI wa Kata ya Tabata, Omary Matulanga ameeleza Mikakati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Dkt.Samia Suluhu Hassan katika miradi ya maendeleo ambayo inaelekezwa kata ya Tabata
Diwani Omary Matulanga alisema hayo Tabata katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli .
“Serikali ya Dkt samia suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM kata ya Tabata mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji DMDP unatarajia kuanza hivi karibuni mwezi Agosti mradi huu wa DMDP ukianza utaifungua Tabata Barabara za ndani muhimu zitajengwa kwa kiwango cha lami na kiwango cha zege” alisema Matulanga
Diwani Omary Matulanga, alisema Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli ,amekuwa mkombozi katika kutatua kero jimboni sasa hivi Barabara ya Kimanga,Kisiwani,kutokea Savana ikikamilika itakuwa mkombozi upembuzi yakinifu umekamilika .
Alisema daraja la Kisiwani Mwananchi pia litajengwa la kisasa katika mradi wa Kuboresha miundombinu ya jiji DMDP ambapo barabara zote za ndani Tabata zitawekwa na taa katika mradi huo .
Akizitaja barabara zitakazojengwa Tabata Diwani Matulanga alisema barabara tano ambazo baadhi yake ni Magengeni Umoja Road,Tabata shule kwa sesi ,Tabata Mtambani,dampo kutokea Kigogo.
Akizungumzia Mikakati mingine ya Serikali kata ya Tabata ambayo yamefanywa kwa ushirikiano wa Mbunge Bonnah alisema zahanati ya kisasa inajengwa Tabata Kisiwani na sekta ya Elimu Kata ya Tabata wameingiziwa shilingi milioni 240.
Matulanga alisema Tabata wanampa kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi vizuri na kuleta maendeleo kwa kasi Kata ya Tabata sasa inakuwa ya kisasa.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja