January 20, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Mariam awasilisha Ilani ya Chama, ajivunia mafanikio

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Diwani wa Kata ya Mchafukoge Mariam Lulida amewasilisha Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ya Mwaka 2022 /2023 na kujivunia mafanikio makubwa yaliotekelezwa na serikali..

Akizungumza wakati wa kuwasiisha taarifa ya Ilani ya Chama ukumbi wa mikutano Arnatogluo alisema kata ya Mchafukoge inajivunia Serikali ya awamu ya sita katika utekelezaji wa Ilani katika miradi mbalimbali ya Maendeleo .

Akizungumza wakati wa kuwasiisha Ilani alisema kata ya Mchafukoge sekta ya afya Wana hospitali Moja ya Mnazi Mmoja ambayo imepandishwa hadhi Kutoka kituo cha afya na kuwa hospitali ya mkoa ambayo inahudumia wagonjwa wa mkoa Dar es Salaam na mikoa ya Jirani

“Halmashauri ilinunua Mashine ya kuchakata taka zinazotokana na Ward ya kina mama ambapo ilitolewa Pesa takribani shilingi milioni 38 pamoja na Pesa za Ujenzi sehemu ya kukaa wagonjwa wakisubiria kuingia kwa daktari shilingi milioni 40″alisema LULIDA .

Diwani Mariam Lulida alisema pia Ambulance ya kisasa ya kubebea wagonjwa imepatikana kwa msaada wa KOICA yenye thamani ya shilingi milioni 57 na kituo cha mama, mtoto kimegharimu shilingi milioni 200 na generator kwa ajili ya hospitali shilingi milioni 50 .

Akizungumzia miundo mbinu Serikali kuu kupitia LATRA imeboresha standi mbili zilizopo kata ya Mchafukoge Mnazi Mmoja na Stesheni ambapo maboresho hayo yamewezesha kuhudumia magari 143 Stesheni na 762 Mnazi Mmoja kwa Siku .

Aidha Diwani Lulida alisema Serikali pia imekarabati Barabara ya Libya na Mosque shilingi milioni 76 ,uboreshaji wa Bustani ya Mnara wa saa kaburi Moja chini ya Jica shilingi Bilioni 1 .

Akizungumzia Barabara za TARURA alisema uzibaji wa mashimo katika barabara za LIBYA. JAMHURI. AGREY. INDIA. SOPHIA KAWAWA na Barabara za TANRODS ukarabati wa kingo za barabara ya NYERERE , UHURU. STESHENI NA NKRUMAH.

Alitoa shukrani kwa viongozi wa chama Cha mapinduzi CCM ngazi ya Kata ,Wilaya, Mkoa hadi Taifa pamoja na wanachama wenzake Wananchi wa Kata ya Mchafukoge kwa ushirikiano wao kumwamini katika kuongoza Kata hiyo wakiwemo madiwani wa Halmashauri ya Jiji ,Meya wa Halmashauri Omary Kumbilamoto na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu .

Kabla kuwasilisha Ilani Diwani Mariam Lulida alianza na Semina elekezi kwa Wenyeviti (Mabalozi )na Wajumbe wa Mashina kwa kata nzima na Wenyeviti mabalozi wa Jimbo lote la Ilala.

DIWANI wa Kata ya Mchafukoge Mariamu Lulida akiwa na DIWANI wa Ilala Saady Kimji wakati wa kuwasilisha Ilani ya Chama ya mwaka 2022 mpaka 2023 Picha na Heri Shaaban.
Viongozi wa kata ya mchafukoge wakiwa katika Picha ya pamoja Diwani wa kata hiyo Mariam Lulida na Diwani wa Ilala Saady Kimji wakati wa kuwasilisha Ilani ya chama (Picha na Heri SHAABAN )