July 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Malisa awataka wanakiwalani kumlinda Kafana

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu Godlisten Malisa, amewataka wananchi wa Kata ya Kiwalani wilaya ya Ilala kulinda adhina ya Kiwalani ya Diwani wa Kata hiyo Mussa Swed Kafana, kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi vizuri na utendaji bora wa kazi.

Diwani Godlesten Malisa ,alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kiwalani wakati Diwani Mussa Kafana alipokuwa akiwasilisha utekelezaji wa Ilani aliyofanya katika uongozi wake.

“Kiwalani sasa imekuwa Ulaya ndogo ina kila kitu zikiwemo huduma za kijamii,kituo cha afya,shule,masoko na miundombinu ya Barabara mwanzo mambo haya yalikuwa hakuna wananchi wa Kiwalani na wana chama wa chama cha Mapinduzi tumtumie vizuri Diwani Mussa Kafana ,aendelee kuongoza Kiwalani tusisikilize maneno ya Wana SIASA waliomaliza muda wake kumchafua Diwani wenu aliyopo madarakani wasiwafuate wapaka poda wa kiume.

Diwani Malisa alisema Diwani Musa Kafana amefanya mambo makubwa katika kata ya Kiwalani kwa kushirikiana na Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ,sasa hivi Kiwalani maendeleo makubwa wamepata sekta ya afya,sekta ya Elimu na Miundombinu ya Barabara hivyo hivyo wana siasa uchwara wanaochafu viongozi waliopo madarakani wasiwasilkilize badala yake Kiwalani wametakiwa kushirikiana na viongozi waliopo madarakani katika kuleta maendeleo

Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Vingunguti Mohamed Mluya amewataka Kiwalani kutumia akili zao vizuri kwani kuna watu wamesoma lakini mashuleni hawana akili .

Katibu wa Mbunge wa jimbo la segerea Lutta Lucharaba, alitoa taarifa kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ambapo Lucharaba alisema jimbo la segerea Kiwalani na Minazi Mirefu ndio yenye Barabara za kisasa na sasa ameomba Barabara nane za kisasa ,lakini katika Jimbo hilo Kimanga,Kisukuru na Buguruni amna Zahanati Kiwalani huduma zote zipo mpaka kituo cha afya cha kisasa na sasa Serikali imeelekeza Shilingi bilioni 1 ya sekta ya Elimu kwa ajili ya sekondari ya Gholofa.

Diwani wa Kata ya Kiwalani Mussa Kafana, alisema Uongozi wa Kata ya Kiwalani na Serikali wanaendelea kushirikiana na viongozi wa chama cha Mapinduzi Wastaafu kwa ajili ya ushauri na kuleta maendeleo ya kata hiyo.

Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi Kiwalani alisema mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji DMDP awali walipata Barabara 12 awamu ya pili walikosa Barabara za mradi huo kwa sasa wamepata Barabara nane wanampongeza Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli kwa kuwapigania kupata Barabara hizo.

Akizungumzia mafanikio mengine Musa Kafana alisema Dkt Samia Suluhu Hassan amejenga kituo cha afya cha Kisasa Kiwalani pamoja na Huduma za mama na Mtoto huduma zote zinapatikana hivyo aliwataka Kiwalani kumuunga mkono Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya makubwa.