November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Lulida afanya ziara katika mradi wa reli ya kisasa SGR

Na Heri Shaaban

, TimesMajira Online, Ilala

Diwani wa Kata ya Mchafukoge MARIAM LULIDA, na Kamati ya Siasa ya Kata ya Mchafukoge, wananchi wa Kata hiyo Wafanyabiashara wamefanya Ziara katika mradi wa reli ya kisasa SGR katika madhimisho ya kuzaliwa CCM kutimiza miaka 46 .

Katika ziara hiyo Diwani Mariamu Lulida na Kamati ya Siasa ya Mchafukoge walianza ziara hiyo makao makuu ya SGR Stesheni mpaka Stesheni ya Pugu wilayani Ilala kujionea miradi mkakati ya Serikali ya awamu ya sita inayotelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika ziara hiyo Diwani wa Kata ya Mchafukoge Mariamu Lulida alimshukuru Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan, kwa kutekekeza Ilani miradi mikubwa ya Maendeleo yenye fursa Katika nchi yetu Tanzania ya uchumi wa viwanda .

“Kamati yangu ya Siasa ya kata Mchafukoge ,Wafanyabiashara viongozi wa chama tumekagua miradi mkakati ya Serikali Rais wetu ametoa trioni 14 ni sehemu ya kujivunia kata ya Mchafukoge ” alisema Lulida .

Diwani Maliam Lulida alisema Katika madhimisho ya CCM kutimiza miaka 46 ya CCM viongozi wa chama wote wamejionea miradi hiyo mikubwa wamepanda treni ya mabehewa mapya ya kisasa wamejionea hivyo wataenda kueleza mazuri kwa Wananchi .

DIWANI Lulida alisema Serikali ya awamu ya sita Rais wetu anafanya kazi kubwa sana katika utekekezaji miradi ya Maendeleo ikiwemo Afya sekta ya elimu,barabaraKatibu wa Siasa na Uwenezi wa Kata ya Mchafukoge Mshokery Mandary alisema amejifunza mengi katika mradi wa SGR atakuwa na sehemu ya kuzungumza kwa wananchi kuhusiana na mradi huo mkubwa Serikali waliowekeza wenye thamani ya shilingi trioni 16 .

Mandary alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan katika kujenga nchi ya Tanzania ya Uchumi wa viwanda amewataka Wanachi kufanya ziara katika mradi huo kujifunza .

Mwenyekiti wa CCM Mchafukoge Jammar Abubakar alipongeza Serikali ya Jamhuri ya MUUNGANO wa Tanzania kazi nzuri imefanyika na mabehewa yote mapya yapo Pugu tayari kwa kuanza safari .

MHANDISI Meneja Mradi Msaidizi kipande Cha Kwanza Dar es Salaam Morogoro David Msusa alisema ujenzi wa reli ya kisasa SGR Dar es Salaam Morogoro karibu unamalizika Mpaka Sasa mabehewa 14 mapya yapo tayari kati ya mabehewa 54.

MHANDISI David alisema reli hiyo ya SGR inatumia nishati ya Umeme wamefikia hatua nzuri mradi wa pili kuelekea Mkoani Mwanza unaanza.

Mhandisi wa Meneja Mradi Msaidizi kipande Cha kwanza Dar es Salaam Morogoro wa SGR David Msusa akizungumza na uongozi wa chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Mchafukoge wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mariam Lulida walipofanya ziara Leo January 30 /2023 katika Madhimisho ya ccm kutimiza Miaka 46(Picha na Heri Shaaban )
Diwani wa kata ya Mchafukoge Mariam Lulida (Kulia )akiwa na kamati ya siasa ya Kata ya Mchafukoge Leo January 30/2023 katika ziara ya kutembelea mradi wa SGR wakati wa kuelekea Miaka 46 ya. CCM (PICHA NA HERI SHAABAN)
Viongozi wa CCM wa Kamati ya siasa Kata ya Mchafukoge wakiwa Katika ziara ya kuangalia mradi wa SGR Stesheni ya Pugu Stesheni Wilayani Ilala Leo January 30/2023 katika Madhimisho ya Miaka 46 ya kuzaliwa CCM