November 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Kwezi awasilisha Ilani, ajivunia mafanikio

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Diwani wa Kata ya Kipawa Kwezi awasilisha ILANI ya chama cha Mapinduzi CCM na kuelezea mafanikio ya Kipawa sekta ya Elimu Halmashauri ,wahisani na Wananchi kwa ujumla wamepokea kiasi Cha shilingi 837,457,800 katika kutekekeza miradi mbalimbali katika sekta ya Elimu kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa .

Diwani Aidan Kwezi alisema pia kiasi cha shilingi 112,521,365 zimetumika kugharamia Shughuli za utawala katika shule za msingi katika kipindi cha 2020 2022 .

Diwani Aidani alisema pia wamepokea Jumla ya shilingi 52,427,125 kwa ajili ya Elimu Maalum shule ya Msingi Air wing.

Aidha Diwani Aidan Kwezi alisema mafanikio mengine Kata ya KIPAWA sekta ya Elimu Msingi shule ya Msingi Majani ya Chai imekuwa English Medium kwa Sasa inafundisha katika mtaala wa Lugha ya Kingereza kuanzia January 2023

Alisema Idara ya Elimu sekondari zimeingia shilingi 529,402 ,200 lwa ajili ya Ujenzi wa madarasa pia shilingi 343,340,665 zimetumika katika ujenzi wa mdarasa ya sekondari kuanzia 2022 mpaka 2023.

Alisema shule ya sekondari Ilala shilingi Milioni 80,000,000 zimetumika katika ujenzi wa madarasa manne fedha za pochi la mama shule ya sekondari Minazi mirefu shilingi 160,000,000 zimetumika kujenga vyumba nane vya madarasa chanzo Cha pesa za Mkurugenzi .

Mwenyekiti wa Chama Cha Màpinduzi CCM WIlaya ya Ilala Saidi Sidde alisema kata ya Kipawa ni kata kubwa na Viongozi wa Kipawa wote wana uwezo ambapo aliwataka wote kukitetea chama cha Màpinduzi CCM Ili kiweze kuendelea kushika Dola .

Mwenyekiti Said Sidde alisema kata ya Kipawa ni kata ya kisasa ina Miradi mikubwa ya maendeleo ambayo imetekelezwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Kuhusu kero za Kipawa Bonde la Mto Msimbazi na SOKO la Kipawa Serikali itatatua hivi karibuni kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli .

Aliwataka viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama ndani ya Chama na nje ya Chama katika Utekelezaji wa Ilani .

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kipawa Saidi Mkuwa amewataka viongozi wa Chama Kipawa KUJENGA umoja na mshikamano wawe wamoja kusaka Dola na kufanya kazi za Chama na Serikali .

Diwani wa kata ya Kipawa IDAN Kwezi akikabidhi Ilani ya utekelezaji wa chama Kwa MWENYEKITI wa CCM wilaya ya ILALA Said SIDDE Katika Kikao Cha Wajumbe wa Halmashauri kata ya KIPAWA February 25/2023 (Picha na HERI SHAABAN
Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Magreth Cheka akizungumza katika kikao Cha Halmashauri Kuu Kipawa February 25/2023 wakati Diwani wa kata ya Kipawa Idan Kwezi alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama (Picha na Heri Shaaban )
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kipawa Mwanahamis Shaban akizungumza Katika Kikao Cha Halmashauri Kuu wakati Diwani wa Kipawa Idan Kwezi alipokuwa akiwasilisha TAARIFA ya utekelezaji wa Ilani
Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli akitoa ufafanuzi kuhusiana na malipo ya Fidia Kwa wakazi wa Kipunguni Kwa ajili ya kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege katika kikao Cha HALMASHAURI Kuu KIPAWA February 25/2023 (Picha na Heri Shaaban. )