Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
DIWANI wa Viti Maalum wilaya ya Ilala Aisha Kipini, amesema Sukari ipo ya kutosha nchini baadhi ya wafanyabishara walificha sukari hiyo na kuongeza mfumo wa bei kwa ajili ya kuikomoa Serikali.
Diwani Aisha Kipini ,alisema hayo Kata ya Ilala katika mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM mtaa wa Karume ya mwaka 2019 mpaka 2024 iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa karume Hajji Bechina.
“Wananchi sukari ipo ya kutosha katika nchi yetu tunaomba msimame imara kuisemea Serikali kwa jamii Tanzania hakuna shida ya sukari ni makundi ya Wafanyabishara wameificha bidhaa hiyo sokoni kupelekea mfumuko wa bei”alisema Aisha
Aliwataka wana CCM Ilala kusimama imara kumsemea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM na kuleta fursa ya maendeleo katika nchi yetu
Alisema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa katika jimbo la Ilala kata ya Ilala kwa kuwekeza sekta ya Elimu imejenga shule za msingi na sekondari katika sekta ya afya amejenga vituo vya afya na zahanati za kisasa na sasa hivi miundombinu ya Barabara ujenzi wake unaendelea ambapo yote yanafanyika katika usimamizi wa uongozi wa Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu na Diwani wa Kata ya Ilala Saady Kimji.
Diwani Aisha Kipini alisema kata ya Ilala inatarajia kugeuka kuwa ulaya ndogo kwa mambo aliyofanya Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo ameanza ujenzi wa Barabara za kisasa,amejenga vituo vya afya vya kisasa sekta ya afya,sekta ya elimu amejenga shule za Msingi na sekondari na sasa mikakati yake kujenga masoko ya kisasa.
More Stories
Tanga kutumia vituo 5405,kupiga kura leo
NMB yatoa msaada wa vifaa Mufindi
Viongozi wa dini Katavi waomba wananchi kujitokeza kupiga kura