Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salam diwani wa Ilala Saady Kimji amesema mikakati yake mwaka huu kutokomeza ZIRO Sekta ya Elimu Sekondari Kata ya Ilala.
Diwani Kimji aliyasema hayo Dar es Salam jana wakati wa hafla ya kupokea viti 100 na Meza Elimu Msingi vilivyotolewa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Boma HAJI BECHINA mlezi wa kata ya ILALA Sekta Elimu.
“Taarifa ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Boma Haji Bechina inaeleza mafanikio ya Elimu Msingi Shule ya Ilala Boma na Mkoani Wanafunzi wamefaulu asilimia 100 wamekwenda kidato cha kwanza Mwaka huu wengi upande wa Elimu sekondari wanafunzi wetu wamefanya vibaya hivyo mikakati yangu ya Kata hii ya Ilala kutokomeza ZIRO Elimu sekondari “alisema Kimji
Diwani Kimji alisema mpango wa elimu tokomeza ZIRO ulizinduliwa Kisarawe Mkoa wa Pwani na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Joketi Mwegelo umeleta mafanikio makubwa Mkoa wa Pwani wameweka kipaumbele Elimu kwa sasa.
Kimji alisema mikakati hiyo ya tokomeza ZIRO llala itakuwa endelevu Wazazi kwa kushirikiana na Walimu ili kuakikisha ufaulu unaongezeka na taaluma shuleni inakuwa.
Alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ILALA Boma Haji Bechina kwa msaada aliotoa wa viti 100,meza na Televisheni pamoja na kingamuzi shule ya Msingi Ilala Boma na Mkoni.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Ilala Boma Haji Bechina alisema yeye ni Mlezi wa shule hizo ndani ya kata ya Ilala msaada aliotoa ni sehemu ya kupunguza changamoto na kuunga mkono juhudi za serikali katika mpango wa Elimu bure.
Mwenyekiti Bechina alisema kila mwaka shule za msingi ILALA Boma na Mkoni zinafanya vizuri matokeo ya Elimu Msingi changamoto iliyokuwepo Wanafunzi wa shule za sekondari wanamuanguasha anaomba Wazazi washirikiane kwa pamoja kuakikisha wanafunzi wetu wanafanya vizuri ufaulu unaongezeka.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo Almasi Kasongo alipongeza Uongozi wa Serikali ya Mtaa Ilala Boma pamoja na Mwenyekiti Haji Bechina kwa Msaada huo na kukuza Sekta ya Elimu Tanzania kwa kuweka mazingira ya kujifunzia na kusoma vizuri katika shule hizo
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu