Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
DIWANI wa Kata ya Ilala Saady Kimji ,amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi( CCM) kwa kipindi cha 2023 mpaka 2024.
Akizungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya kata ya Ilala wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani SAADY KHIMJI, alisema katika kipindi hicho baadhi ya mambo mbali mbali aliyotekeleza yakiwemo sekta ya afya Ujenzi wa zahanati ya Bungoni umegharimu shilingi 358,000,000 Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Afrika Relief Organization kwa kushirikiana na Ubalozi wa Kuwait pia uboreshaji wa zahanati hiyo kwa sasa imekuwa ya kisasa ina vifaa vya kisasa ikiwemo Utra Sound .
“Kata yetu ya Ilala kwa sasa ina Zahanati ya kisasa ina toa huduma masaa 24 ikiwemo huduma za mama na Mtoto MCH ,pia sekta ya elimu Ilala tumejenga shule saba za msingi ikiwemo shule ya Msingi Amana,Ilala Boma,shule ya Msingi Ilala,shule ya Msingi Mkoani,Msimbazi ,Msimbazi Mseto,na shule ya Msingi MZIZIMA ya English Medium “alisema Khimji.
Diwani Kimji akiekezea shule za Sekondari alisema kata ya Ilala katika uongozi wake imefanikiwa kujenga shule tano kati ya hizo za Serikali tatu ambazo ni Sekondari ya Msimbazi,Mivinjeni na Ilala Kasulu shule Binafsi Ilala Islamic na Dar es Salaam Islamic .
Akizungumzia lishe alisema Kata ya Ilala kupitia Afisa Mtendaji wa kata hiyo wanaendelea kuakikisha watoto wote wanapata lishe bora pia wanafunzi wanapata lishe Bora wakiwa shuleni na Familia zinaelimishwa kutoa elimu ya lishe sambamba na ugawaji wa Bima za Afya wamefanikiwa kugawa bima za afya kwa wananchi 315 na kugawa vifaa vya watoa huduma za afya za msingi.
Akizungumzia Sekta ya maji alisema wananchi wa kata ya Ilala wanaendelea kupata maji safi na salama kutoka DAWASA pia visima vya watu Binafsi ambapo Serikali inaendelea kutoa dawa ya kutibu .
Aliwataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya kata ya Ilala kujenga umoja na Mshikamano katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ilala Habib Nasser pamoja na wajumbe wake wa Halmashauri Kuu wamepongeza Utekelezaji wa Ilani uliofanywa na Diwani Kimji ambapo wajumbe wote walifanya ziara kuangalia miradi ya Serikali iliyopo ndani ya kata ya Ilala wamelizia.
Akizungumza katika utekelezaji wa Ilani Mwenyekiti Habib Nasser alisema yeye na Wajumbe wake wa Halmashauri kuu wamekagua miradi ya maendeleo ya Serikali kuangalia fedha za Serikali zinavyofanya kazi
“Wajumbe wa Halmashauri Kuu naomba umoja na mshikamano katika kata yetu Ilala tuweze kuilinda miradi ya Serikali iliyotelekezwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano wa Mbunge wetu Mussa Zungu na Diwani wetu wa Ilala Saady Kimji sasa hivi Ilala tunajivunia kuna viwanja vya michezo vya kisasa,shule ya kisasa ya English Medium na zahanati huduma zote za kijamii zinapatikana Ilala “alisema “Habib.
More Stories
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais
NIDA yawakumbusha wananchi kuchukua vitambulisho vyao