Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Diwani wa Kata ya Ilala Saady Kimji , ambaye ni Mjumbe wa Baraza la Wazazi CCM Taifa amesema Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kalume Hajji Bechina, anatosha kuendelea na uongozi wake wa Serikali ya Mtaa Kalume viatu alivyovivaa vinamtosha kuendelea navyo.
Diwani Saady Kimji ,alisema hayo mtaa wa Kalume wakati Mwenyekiti Hajji Bechina ,alipokuwa akigawa kadi za Bima ya afya kwa wananchi wake 300 wa mtaa huo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali pamoja na meza 30 za Walimu wa shule ya Ilala Boma na Mkoani.
” kazi zinazofanyika kata ya Ilala tukikutana katika mitaa mingine yote tutaenda kuyaekeleza Kamati ya kata Tunajivunia utekelezaji wa Ilani ya chama Serikali ya Mtaa Kalume amewataka Wenyeviti wengine kuiga mfano wa Mwenyekiti Hajji Bechina anauoiga mwingi na kuunga mkono juhudi zake viatu alivyovaa vinamtosha akuna mtu mwingine ataviweza kuvaa Haji Bechina na Wajumbe wake wa Serikali ya mtaa wanafanya kazi vizuri ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi “alisema Kimji
Diwani Saady Khimji alisema utekelezaji wa Ilani ya ccm Mtaa wa Kalume kwa ushirikiano wao viongozi wa kata wanafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akielezea utekelezaji wa Ilani kata ya Ilala katika uongozi wake baadhi ya mambo aliyotekeleza alisema katika sekta ya Elimu amepokea shilingi milioni 306 imeenda kujenga shule za msingi za kisasa na madarasa ya shule za awali ,jengo la Utawala ambapo kazi zinazofanyika kata ya Ilala
Akieleza mikakati mingine ya kata ya Ilala kwa juhudi za Mbunge wa Ilala Mussa Zungu na Serikali wanajenga soko la kisasa Ilala Boma litakuwa kama soko la Kariakoo au Kisutu na Barabara za ndani zinajengwa kwa kiwango cha lami baadhi ya Barabara Mkandarasi ameanza Mtaa wa Moshi ambapo alisema yale yote ambayo ametoa ahadi katika utekelezaji wa Ilani anaenda kutekeleza.
Aidha alisema katika miradi ya sekta ya afya katika kata ya Ilala wanatarajia kujenga zahanati ya kata itajayotumiwa na wakazi wa eneo hilo ili kuondoa usumbufu wa kwenda hospitali ya Rufaa Mkoa AMANA.
Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu, kwa ushirikiano mkubwa anaotoa Ilala pamoja na Mwenyekiti wa chama wilaya Said Sidde na Kamati yake ya siasa Wilaya.
Pia alimpongeza Mtendaji wa Mtaa Kalume anatoa ushirikiano mkubwa katika kutatua changamoto za wananchi pamoja na kuisaidia Serikali kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi.
More Stories
Nani kuwa mrithi wa Kinana CCM?
Watendaji Songwe wapatiwa mafunzo uboreshaji daftari la mpiga kura
Samia: Mwaka 2024 ulikuwa wa mafanikio