July 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Fatuma awasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Diwani wa Kata ya Gerezani Fatuma Abubakari, amewasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2023 mpaka 2024 kwa kuelezea yale aliyofanya katika uongozi wake.

Diwani Fatuma Abubakari, alisema katika kipindi cha uongozi wake baadhi ya mambo aliyoyafanya ya utekelezaji wa Ilani sekta ya Elimu Dar es Salaam Sekondari madarasa matano ,Gerezani Sekondari madarasa manne ,shule ya Benjamini William Mkapa madarasa mawili ,sekondari ya Uhuru Mchanganyiko madarasa matano jumla madarasa 16 Uhuru Mchanganyiko matundu kumi ya vyoo pamoja ujenzi wa mabweni jiko vyoo solar .

Aidha alisema pia Benjamini William Mkapa ujenzi wa maktaba na ukumbi pamoja na Uwekeji wa nyasi Bandia pesa kutoka Serikali kuu na Halmashauri mapato ya ndani .

“Katika utekelezaji wa Ilani pia kwa upande wake shule za msingi shule ya Gerezani ukarabati wa paa jipya ,uhuru Wasichana ukarabati wa vyoo pamoja na kituo cha Walimu TRC ” alisema Fatuma.

Diwani Fatuma Abubakari alisema pia kwenye upande wa Miundombinu ujenzi wa barabara Kiwango cha Lami Barabara ya Kipata Livingstone na Nyamwezi na Barabara ya Makamba na Viwandani . na Gerezani fedha kutoka Serikali kuu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania TANRODS na mapato ya ndani Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.

Akizungumzia mafanikio yake katika kipindi hicho katika upande wa sekta ya afya alisema Zahanati ya Gerezani uchimbaji wa Visima na ukarabati wa vifaa tiba kwa kushirikiana na Wadau wa afya Albarakah Foundation na Mdau Bora Fhamacy.

Aliwataka wananchi wa Gerezani kushirikiana na chama na Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ili kifikie malengo yake ya kushika dola.

Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala ASHA JOHARI alisema Rais wa awamu ya Sita Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa hivyo wananchi wa Ilala na Gerezani kwa ujumla tuunge mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi anazofanya Jimboni Ilala