Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Mwalimu Beatrice Edward amewataka walimu Ilala kufanya kazi kwa weledi kushirikiana na Walimu kutokomeza ZIRO.
Mwalimu Beatrice ametoa ushauri huo katika kikao cha Kamati ya Maendeleo Kata ya Ilala kilichokuwa kinajadili Maendeleo .
“Nawaomba Walimu wenzangu tushirikiane na wazazi katika Sekta ya elimu kuisaidia Serikali kutokomeza ZIRO Ilala iweze kuwa juu kwenye Eimu” alisema Mwalimu Beartice
Aliwataka Walimu kuendelea kusimamia maadili kwa Wanafunzi wawapo shuleni na Walimu wa shule za Sekondari kuiga mfano Elimu Msingi katika jitihada za kuongeza ufaulu
Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Aisha Kipini, aliwataka Wazazi kutenga muda kuzungumza na watoto wao wawe marafiki kila wakati kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili .
Aidha Diwani Aisha alipiga MARUFUKU wazazi kutuma watoto sokoni na dukani nyakati za usiku kwani ulimwengu umebadilika watu wanawafanya vitendo Vya ukatili watoto .
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa