Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
DIWANI wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Dkt.Julieth Banigwa, amewataka Maafisa Kulimo , kufanya kazi kutoka kwenda kuwahudumia wananchi mashambani wasikae maofisini.
Dkt. Julieth Banigwa alisema hayo Kata ya Mzinga Wilayani Ilala wakati wa kugawa vifaa vya kilimo kwa Wanawake wa Mboga mboga ili waweze kuvitumia mashambani.
“Maafisa Kilimo kazi yenu kubwa kutembelea mashambani kutoa elimu na wakulima wetu ili waweze kuboresha kilimo chao msikae ofisini ” alisema Dkt.Banigwa.
Dkt Julieth Banigwa akizungumza na Wanawake Wakulima wa Mzinga aliwataka watumie vifaa hivyo vya Kilimo kwa ajili ya kuboresha biashara zao na kukuza sekta ya Kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Dkt. Julieth Banigwa, alisema anaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha Wanawake Kiuchumi ili waweze kusonga mbele.
Aidha kwa upande Mwingine aliwataka wanawake wa Kata Mzinga kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura waweze kupata haki yao ya Msingi kuchagua viongozi bora .
Katika upande Mwingine alitumia fursa hiyo kugawa kadi za chama na uwt kwaajili ya kuongoza wanachama wapya wa Jumuiya ya wanawake.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba