DIWANI TUMIKE MALILO AELEZA MAFANIKIO NA KUMSHUKURU RAIS
Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar
DIWANI wa Kata ya Bonyokwa Tumike Malilo, ameeleza mafanikio yake katika uongozi wa Udiwani ndani ya kata ya Bonyokwa pamoja na kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuiwezesha Kata ya Bonyokwa kujengwa barabara za ndani kwa kiwango cha lami.
Diwani Malilo alizungumza hayo kata ya Bonyokwa wilayani Ilala leo wakati wa kikao maalum alipokuwa akikabidhi sare za ulinzi Shirikishi wa kata ya Bonyokwa, kulipia kadi za Bima kwa pikipiki tatu za chama cha Mapinduzi kwa ajili ya umoja wa vijana pamoja na kukabidhi mifuko ya cementi kwa viongozi wa dini sehemu ya ahadi yake ya utekelezaji wa Ilani ambapo alitumia fursa hiyo kuelezea maendeleo aliofanya kwa kushirikiana na Mbunge wa Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli.
Diwani Tumike Malilo alisema katika Udiwani wake hichi ni kipindi cha pili maji na miundombinu ya barabara ametekeleza kwa kushirikiana na Mbunge wa Segerea changamoto kwa sasa zimeisha.
“Namshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mbunge wangu Bonah Ladslaus Kamoli, miundombinu ya barabara inajengwa kwa kiwango cha lami mpaka Bonyokwa standi, na barabara ya Bonyokwa Kinyerezi kwenda Kimara inajengwa ya kisasa pamoja na kufungwa taa ni kazi kubwa hii imefanywa na Serikali katika utekelezaji wa Ilani yangu”alisema Tumike.
Tumike alisema barabara zingine zinazojengwa kwa kiwango cha lami kwa Masia,Kanada mita 500 muda wowote ujenzi wake unaanza kwa sasa mwanasheria anafatilia taratibu na barabara ya kwa Bi Timdwa inajengwa na Mbunge kwa fedha za mfuko wa jimbo na barabara ya sedafa na pesa nyingine imetoka hivi karibuni inajengwa kupitia kanisa
Akizungumzia sekta ya Elimu Bonyokwa Serikali imejenga madarasa saba ,na sekondari sekondari inajenga shule ya sekondari ya golofa tano na pesa nyingine inajenga madarasa sita na maabara kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha sita .
Kwa upande wake Katibu wa umoja wa vijana Bonyokwa Lucy Joseph Mbwalo ,alimpongeza Diwani wake wa Bonyokwa kwa utekelezaji wa Ilani vizuri ukiwemo kuwalipia vijana wa Bodaboda bima ya jumla ya pikipiki tatu za chama cha Mapinduzi CCM zilizotolewa hivi karibuni kwa ajili ya shughuli za chama.
Lucy Joseph mbwalo alisema Tumike amefanya kazi kubwa Bonyokwa kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo vijana wote wa Bonyokwa wanaelekeza kura zao Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Bonnah Ladslaus Kamoli na Diwani wao Tumike Malilo.



More Stories
Wanafunzi Ilala Boma wafanya ziara ya Masomo uwanja wa ndege
Nishati ya umeme jua kupunguza gharama za uzalishaji migodini
Rais Samia atoa bil.10 ukarabati barabara za ndani Ilala