November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DIT inavyorahisisha ajira kwa vijana

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), imesema ili kukabiliana na sokonla ajira hususan kwa vijana inatoa kozi mbalimbali za muda mrefu na mfupi Ili kutoa fursa kwa vijana kukabiliana na soko la ajira na kuwawezesha kujipatia kipato.

Akizungumza Jijini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri kwenye maonesho ya wiki ya Ubunifu Kitaifa (IWTZ), Mwalimu wa DIT Tawi la   Mwanza Idara ya teknolojia Bidhaa za ngozi Leonard Mayunga amesema chuo hicho kimekuwa kikizalisha vijana wenye ujuzi ambao wanaweza kuajiriwa na kujiajiri wenyewe.

Kwa mujibu wa Mayunga  ,  kiwanda cha Kilimanjaro Moshi nguvu kazi kubwa imetoka katika  Chuo DIT Tawi la  Mwanza na kwamba vijana wao wanapomaliza wanapata ajira katika taasisi na viwanda vilivyopp hapa nchini.

Amesema kuwa katika maonesho hayo wamekuja na  bidhaa mbali mbali  za ngozi zikiwamo viatu,mipira, wallet, mikanda zinazozalishwa katika Chuo cha DIT Tawi la Mwanza.

Akizungumza kuhusu  upatikanaji wa malighafi amesema Tanzania katika Bara la Afrika inashika nafasi ya pili kwa kuwa na mifugo mingi hivyo malighafi hapa nchini inapatikana.

Kwa upande wa bidhaa za mipira amesema wamekuwa wakifanya kazi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),ambapo hivi karibuni shirikisho hilo lilipaleka watu kutoka mikoa mbalimbali ili kujifunza kutengeneza mipira.

“Soko la mipira lipo tayari tumeshanza  kuuza katika timu za mpira zilizopo Jijini Mwanza  naamini hata timu kubwa kama Simba na Yanga nao watakuja tuwauzie bidhaa hii imetengenezwa kwa ustadi mkubwa,” amesema Mayunga.

Aidha amesema,zipo changamoto zinazowakabili ikiwemo matumizi ya mashine za kizamani katika kufanya kazi zao lakini hata hivyo matatajio Yao ni kuwa na mashine za kisasa Ili kurahisisha utendaji wa kazi zao.