Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke ndugu Elihuruma Mabelya amewatoa hofu Wananchi juu ya utoaji wa mikopo ya 10% kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.
Akijibu swali aliloulizwa na mmoja wa waandishi wa habari alipotembelea banda la Manispaa hiyo Agosti 4,2022 katika maonesho ya Wakulima(Nanenane) mkoani Morogoro,Mkurugenzi Mabelya amesema kuwa taratibu zote za utoaji wa mikopo hiyo hufuatwa.
“Nikuhakikishie kuwa utoaji wa mikopo upo wazi,hakuna kikundi chochote kinachopendelewa, utaratibu unaanzia kwenye kata husika , kikundi kinatakiwa kiandae andiko na kwa kifupi ni kwamba utoaji wa mikopo hii hufuata sheria na kanuni”.Alisisitiza Mabelya.
Mabelya ametoa ufafanuzi huo wakati ambapo kumekuwa na taarifa nyingi za upotoshaji kuhusu utoaji wa mikopo hiyo kuwa inatolewa kwa upendeleo.
Awali akikagua baadhi ya shughuli zinazofanywa katika banda la Manispaa ya Temeke,mkurugenzi Mabelya alionesha kufurahishwa kwake mara baada ya kupata maelezo ya kina kutoka kwa wataalamu wa kilimo,mifugo na Uvuvi.
Moja ya matunda ya mikopo inayotokana na 10% ya mapato ya ndani ya Manispaa ni Wajasiriamali ambao wameshiriki katika maonesho ya Nanenane mkoani hapa, ambapo wameweza kuleta bidhaa zao kuzitangaza na kuuza ili kujiongezea mapato.
More Stories
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu