January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamishna General Mamlaka ya madawa ya kulevya nchini Gerald Kusaya Akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo jijini Dar Es Salaam .

DCEA yajipanga kukomesha biashara haramu nchini

Na David John,timesmajira,Online

KAMSHINA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA), Gerald Kusaya ametoa onyo   kali kwa watanzania na Raia wa kingeni wanaoendelea  kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya huku akisisitiza kuwa Mamlaka hiyo aitalala itafanya kazi usiku na mchana.

Kamshina Jenerali Kusaya ameyasema hayo mapema leo Mkoani Dar es salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema DCEA ipo kwa ajili ya mapambano na awatalala usingizi bali watatumia weledi, maisha yao pamoja na nafasi zao ili kukomesha vita ya madawa ya Kulevya nchini.

Amesema  sasa ni wakati muafaka ambao Mamlaka hiyo itafanya kazi kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo nchini.

“DCEA pamoja na vyombo vyote vya ulinzi na usalama tumejipanga vizuri katika kuhakikisha vita ya madawa ya Kulevya tunaishinda”amesema na kuongeza

” Niwahakikishie kuwa kwa jinsi tulivyojipanga tutakuwa washindi katika vita hii”alisisitiza Kamshina Jenerali Kusaya

Aidha amesema katika mapambano hayo DCEA itashirikiana pia na vyombo vingine vilivyo nje ya nchi, Taasisi binafsi za umma ambazo kwa kiasi kikubwa zitasaidia katika mapambano pamoja na wananchi kwa ujumla.

Ametoa  wito kwa watanzania wote wenye mapenzi mema kushirikiana na DCEA katika mapambano ya vita ya madawa ya Kulevya kwa kutoa taarifa huku akiwahaidi kuwa Mamlaka hiyo itatunza siri.