January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dc mpogoro apewa pongezi za Rais na viongozi jamii ya Wamasai ‘Leigwanani’

Na Mwandishi wetu, Timesmajira online

MKUU wa wilaya ya Same Edward mpogoro akipewa pongezi na salaam kwa viongozi wa jamii ya Wamasai leigwanani wakiongozwa na leigwanani mkuu Mussa paulo laizer Kumfikishia Mhe Raisi Mama Samiha Suruhu Hassan kwa upendo wake mkubwa kwao kwa kuwapatia million 500 ya ujenzi wa kituo cha Afya kitu ambacho walikuwa wakiangaika zaidi ya kilometer 55 kwenda kwenye kituo cha Afya kwa miaka yao yote.

Pia kuwatengea Milioni 500 kujenga barabara ya Muungano – Jitengeni kwa kiwango cha Changarawe na kuanza upembuzi yakinifu ya Ujenzi wa Daraja litakalounganisha Wilaya za Same na Sumanjiro. Hivyo wamemuhakikishia DC kumuunga Mkono Mhe. Rais Samia. Kwa kazi nzuri anazo fanya kuleta maslahi mapana kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Same Edward Mpogolo amesema kuwa moja ya sifa ya viongozi bora ni wale wanaojali shida za wananchi wanaowaongoza. Rai hiyo ameitoa jana wilayani humo kwenye sherehe ya kuwasimika viongozi wa kimasai Leigwanani.

Mkuu wa Wilaya ya same Edward mpogoro akimsimika Nginaya Ndeipa kuwa kiongozi wa leigwanani kata ya ruvu wilaya ya Same.

Mpogolo alisema kuwa mmoja wa wanasiasa waliopata kuishi nchini India Mahtma Ghandi alisema kuwa atahakikisha wahindi anaowaongoza wakae kwenye viti kwanza nae atakuwa wa mwisho kuketi. Ikiwa na maana atawatengenezea wananchi wake mazingira ya kuwa matajiri nae atakuwa wa mwisho kupata mali.

Alinukuu kitabu cha TANU na Raia kilichoandikwa na Marehemu baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuhusu kisa cha Mzee Maganga ambaye kuunguliwa na nyumba na chakula baadhi ya viongozi walikwenda kumjulia hali huku bila msaada wowote Lakini Mmoja wao alimsaidia kwa chakula, malazi na mavazi na kusisitiza kuwa huyo anayejua shida za wenzake ndie kiongozi anayehitajika na watanzania.

Hivyo aliwataka shida za jamii ya Masai wa Ruvu wilayani Same iwe shida ya jamii ya wamasai wote Alisema kuwa Mkuu wa mkoa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wameshafikishiwa shida zao zinazowakabili na punde baadhi ya shida hizo zitatatuliwa.

Mpogolo aliwahakikishia wananchi wa Ruvu kuwa kazi ya ujenzi wa Daraja linalounganisha Same na Simanjro itakayosimamiwa na Tarura itaanza mara moja kwa kushirikiana na Wananchi Pia barabara ya Muungano Jitengeni Katika bajeti ya Mwaka huu imetengewa milioni 500 hivyo itatengenezwa juanzia Julai 2022.

Barabara nyingine zitakazotengenezwa ni ile ya Same hadi Ruvu Pia serikali Mkoani humo inafanya jitahada ya kumaliza tatizo la kukabiliana na Tembo waharabifu wa mazao.